Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

First eleven mpya Yanga, Simba kiboko

Wachezaji wa Japan wakishangilia baada ya kuishinda Marekani katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia kwa Wanawake juzi. Japan ilishinda kwa penalti 3-1 baada ya kumaliza muda wa kawaida na dakika za ziada kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.

MWANDISHI WETU USAJILI wa Yanga na Simba sasa unaleta raha. Vikosi vilivyosajiliwa na timu hizo unaweza kutengeneza vikosi viwili kila moja na kucheza kwa fomesheni yoyote ile kutokana na uwezo, uzoefu na ujuzi wa wachezaji hususani waliosajiliwa dakika za mwisho. Makocha Moses Basena wa Simba na Sam Timbe wa Yanga ambao wote ni raia wa Uganda wamesajili viungo, washambuliaji na mabeki wazoefu wa michuano mikubwa kutoka kwenye klabu mbalimbali za Afrika ambao miongoni mwao wametamba kuwa Afrika itawatambua kuanzia ligi ya ndani mpaka nje. Timu hizo ambazo zimesajili kwa gharama kubwa kila moja imeambulia vikosi viwili imara bila kujumuisha watakaobaki kwenye benchi huku moto mkubwa ukisubiriwa katika mechi ya Ngao ya Hisani, Agosti 13 ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ambayo orodha yake ina wachezaji 25, kikosi chake cha kwanza huenda kikawa na mabadiliko makubwa hasa baada ya kupoteza Kombe la Kagame kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga siku kumi zilizopita. Kuna uhakika kuwa kikosi cha kwanza cha Simba langoni ataanza Juma Kaseja, Mabeki; Said Nasoro Chollo, Amir Maftah, Derrick Walulya na Victor Costa wakati kwenye kiungo atasimama Patrick Mafisango, Mwinyi Kazimoto na Uhuru Seleiman. Kwenye ushambuliaji atakuwa Felix Sunzu, Gervais Kago na Haruna Moshi `Boban', hicho ni kikosi cha kwanza. Kikosi cha pili ataanza langoni Ally Mustapha, mabeki Salum Kanoni, Obadia Mungusa, Juma Nyosso na Kelvin Yondani huku Jerry Santo, Shija Mkina na Amri Kiemba wakikamata kiungo. Mastraika wa kikosi hiki ni Mussa Mgosi, Salum Machaku na Ulimboka Mwakingwe wakati ambapo mshambuliaji Rajab Isihaka, Robert Mweta ambaye ni kipa na beki Shomari Kapombe wakisubiri benchi kwa vikosi vyote viwili. Upande wa Yanga, kikosi cha kwanza Yaw Berko atakuwa langoni akilindwa na Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Chacha Marwa na Nadir Haroub `Cannavaro' huku kiungo kikishikiliwa na Juma Seif Kijiko, Nurdin Bakari na Haruna Niyonzima `Fabregas'. Mastraika hapo ni Kenneth Asamoah, Davies Mwape na Hamis Kizza. Muziki wa pili wa Yanga, utakuwa na Shabaan Kado golini, akisaidiwa na mabeki Godfrey Taita, Abuu Ubwa, Job Ibrahim na Bakari Mbegu. Viungo ni Godfrey Bonny, Julius Mrope na Rashid Gumbo wakati Jerry Tegete, Pius Kisambale na Kiggi Makassy watakuwa na kazi ya kushambulia. Wachezaji watano ambao ni Said Mohammed, Salum Telela, Stephano Mwasika, Idrissa Rashid na Fred Mbuna wakisugua benchi.