Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yaifungia Biashara kusajili

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) imeifungia klabu ya Biashara United ya Mara kusajili wachezaji kwa madirisha mawili.
Adhabu hiyo imetolewa baada ya Biashara kushindwa kuheshimu uamuzi wa awali wa FIFA kuifungia kusajili wachezaji hadi itakapokamilisha malipo ya madai ya mishahara ya aliyekuwa mchezaji wake Timoth Balton Omwenga.
Kutokana na kutoheshimu uamuzi huo, ndipo FIFA ilipowasilisha suala hilo katika kamati yake ye Nidhamu ambayo Mei 19, 2022 ilitoa adhabu hiyo kupitia kwa Mjumbe wake Carlos Teran wa Venezuela.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zinaingia na wachezaji pamoja na makocha, kwani hiyo ni moja ya vigezo vya kupata leseni ikiwa ni utekelezaji we Kanuni ya Leseni za Klabu (Club Licensing Regulations).