Fadlu rasmi arithi mikoba ya Manqoba Yanga
Muktasari:
- Kocha huyo amejiunga na Yanga akiwa huru kwa vile hakuwa na timu tangu Juni mwaka huu alipoachana na Raja Casablanca ya Morocco.
Yanga imemtambulisha rasmi Fadlu Davids kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo leo Jumamosi, Novemba 7, 2026.
Kocha huyo amejiunga na Yanga akiwa huru kwa vile hakuwa na timu tangu Juni mwaka huu alipoachana na Raja Casablanca ya Morocco.
Ni Kocha anayemiliki leseni ya ukocha ya ngazi za Juu ya Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (UEFA) ijulikanayo kama UEFA Pro.
Yanga ni timu ya pili hapa Tanzania kwa Fadlu Davids kuifundisha ambapo awali aliinoa Simba.
Akiwa Simba, kocha huyo aliiongoza kufika hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo ilipoteza mbele ya RS Berkane ya Morocco.
Fadlu ni kocha anayependelea kutumia mfumo wa 4-2-3-1.
Kocha huyo anatua nchini leo saa 7:00 usiku akitokea Afrika Kusini tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa Yanga.