Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Damaro aukana uraia wa Tanzania akivunja mkataba Singida BS

DAMARO Pict

Muktasari:

  • Damaro alipewa Uraia wa Tanzania, Januari 2025 yeye sambamba na Emmanuel Keyekeh  na Arthur Bada.

Wakati akitimiza mwaka mmoja na miezi 10 tangu alipopewa uraia wa Tanzania, kiungo Mohamed Damaro ameukana rasmi huku akivunja mkataba na klabu yake ya Singida Black Stars.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Damaro ametangaza uamuzi huo akidai umechangiwa na sababu za kifamilia.

Habari mabibi na mabwana. Nina heshima kutangaza uamuzi wangu wa kuachana na uraia wa Tanzania ambao nilikuwa nimepewa. 

“Nimefikia uamuzi huu kwa sababu binafsi na za kifamilia. Pia, nina heshima kutangaza kusitisha mkataba wangu na Singida Black Star. Nawashukuru wote kwa msaada na ushirikiano wenu,” amesema Damaro.

Januari 2025, Damaro, Emmanuel Keyekeh na Arthur Bada, walitangazwa na Idara ya Uhamiaji kuwa wamepewa uraia wa Tanzania baada ya maombi yao kukubaliwa.

“Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu kupatiwa uraia wachezaji watatu wa timu ya mpira wa miguu ya Singida Black Stars wanaotajwa kwenye taarifa hizo kama ifuatavyo, 1. Emmanuel Kwame Keyekeh 2. Josephat Arthur Bada 3. Mohamed Damaro.

“Wachezaji hao tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.  Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi,” ilinukuliwa taarifa ya Idara ya Uhamiaji.

Ikumbukwe katika kundi hilo, mchezaji mwingine, Arthur Bada hivi sasa anatumia hati ya kusafiria ya nchi yake aliyozaliwa ya Ivory Coast.