Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzungu aibeba Singida BS, ikitibua sherehe ya Mgunda

MZUNGU Pict
MZUNGU Pict

Muktasari:

  • Ushindi huo unaibeba Singida ikipanda kwa nafasi moja kutoka ya tano mpaka ya nne, ikifikisha pointi 10 baada ya mechi zake tano, ikiishusha Mbeya City yenye pointi tisa.

Singida Black Stars imefanikiwa kupata ushindi wa tatu kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Namungo ya Lindi kwa mabao 3-2.

Ushindi huo unaibeba Singida ikipanda kwa nafasi moja kutoka ya tano mpaka ya nne, ikifikisha pointi 10 baada ya mechi zake tano, ikiishusha Mbeya City yenye pointi tisa.

Bao la dakika 71 likifungwa na Marcel  Kanadi raia wa Austria ndio limeamua mchezo huo akifunga kwa shuti kali la mguu wa kushoto mbali na aneo la hatari,akipokea pasi ya Mohammed Damaro.

Bao hilo la Kanadi ambaye alifunga  dakika chache tangu aingie uwanjani akichukua nafasi ya Ahmed Pipino linakuwa la kwanza kwa kiungo huyo tangu asajiliwe na klabu hiyo.

Mapema Singida ikalazimika kutoka nyuma baada ya beki wake Benjamin Tanimu, kujifunga dakika ya 17 akishindwa kuidhibiti krosi ya beki wa kushoto wa Namungo Hance Masoud.

Singida ilisawazisha bao hilo kupitia kwa  Damaro ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo kwa shuti kali dakika ya  45 akipokea pasi safi ya Henry David, timu hizo zilienda mapumziko zikifungana bao 1-1.

Kipindi cha pili, Namungo ilifanikiwa kutangulia tena kwa bao la mkwaju wa penalti ya Rodgers Gabriel dakika ya  49 ikitokana na Redemtus Mussa kuchezewa vibaya na beki Ibrahim Imoro wa Singida .

Singida ilifanikiwa kusawazisha bao hilo kwa mara ya pili kupitia Sagasse Nzaou dakika ya 54 akipokea pasi ya winga wa timu yake Jeancy Mboma.

Mpaka mwisho wa Mchezo Singida imefanikiwa kupata ushindi wa tatu nyumbani huku Namungo ikipoteza mchezo wa pili mfululizo, ikitibua sherehe ya kuzaliwa kwa kocha wake Juma Mgunda.