Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chipukizi yaimarisha kikosi

CHIPUKIZI Pict
CHIPUKIZI Pict

Muktasari:

  • Katika maboresho hayo, ilianza na utambulisho wa kocha ambaye ni Suleiman Mohammed ‘Mani Gamera’ aliyeifundisha Fufuni msimu uliopita.

WAKATI zikisalia takribani siku 20 kuanza Ligi Kuu Zanzibar msimu wa 2026-2027, Chipukizi imeendelea na maboresho ya kikosi chake.

Katika maboresho hayo, ilianza na utambulisho wa kocha ambaye ni Suleiman Mohammed ‘Mani Gamera’ aliyeifundisha Fufuni msimu uliopita.

Katika eneo la kikosi, timu hiyo imetambulisha nyota sita ambao ni Dady Hiluka aliyekuwa mchezaji wa Mtibwa Suger iliyoshiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026 na kushuka daraja.

Wengine ni Kimu Juma, Salum Kifigo, Suleiman Kibadeni, Haruni Ndile na Canille Mgonela.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha wa Chipukizi, Suleiman Mohamed ‘Mani Gamera’ amesema wachezaji hao ni miongoni mwa wanaotazamiwa kufanya makubwa msimu utakapoanza.

Alibainisha kuwa, Chipukizi imeshaanza kujinoa kwa kufanya mazoezi kujiandaa mapema kwani malengo yao ni kutoa ushindani mkubwa.

“Chipukizi ya msimu huu itakuwa tofauti na ilivyokuwa misimu iliyopita kwani tumejipanga kushindana na sio kucheza kwa kufikiria tusishuke daraja kama ilivyozoeleka,” amesema.

Wakati ikiboresha kikosi, kuna wachezaji wameachwa ambao ni Mashir khamis Sabur, Ayoub Moh’d Abdallah, Job Song, Bille Mwakysa, Sadat Abdallah, Omar Kanyoro, Ali Moh’d Ali, Morata, Abdulraut Haji Makame, Mahir Khamis Sabur, Said Suleiman Matar na Shaban Ali Geda.