Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ceasiaa Queens yaibana mbavu Simba Queens nyumbani

Muktasari:

  • Mchezo huo ulikuwa wa raundi ya nne kwa Simba Queens, ambayo iliingia uwanjani ikiwa na rekodi nzuri ya ushindi katika michezo iliyopita.

Simba Queens imebanwa mbavu nyumbani baada ya kutoa suluhu ya bila kufungana na Ceasiaa Queens ya Iringa mechi iliyopigwa leo Novemba 18, 2026, kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam

Mchezo huo ulikuwa wa raundi ya nne kwa Simba Queens, ambayo iliingia uwanjani ikiwa na rekodi nzuri ya ushindi katika michezo iliyopita.

Hata hivyo, safari hii ilishindwa kupata njia ya kuuvunja ukuta wa Ceasiaa Queens, iliyocheza kwa nidhamu na kuhakikisha inatoka na pointi moja dhidi ya moja ya timu zenye nguvu katika ligi hiyo.

Golikipa wa Ceasiaa, Amina Rajabu alikuwa mwiba kwa washambuliaji wa Simba akichomia michomo ya hatari iliyopigwa langoni mwake.

Hii inakuwa  mara 12 tangu timu hizo mbili zilipokutana Oktoba 26, 2019,Kabla ya sare hiyo, Simba Queens ilikuwa imeshinda mechi nane na kutoka sare tatu bila kupoteza hata mmoja.

Katika michezo hiyo 11 iliyopita, Simba Queens ilikuwa imefunga mabao 30 dhidi ya matatu ya Ceasiaa Queens,l. Matokeo yaliyovutia zaidi yalikuwa ushindi wa mabao 15-0 wa Simba Queens uliopigwa  Desemba 23, 2021, ukiwa ni ushindi mkubwa zaidi katika historia ya mechi hizo.

Pamoja na tofauti hiyo kubwa ya mabao, Ceasiaa Queens imeendelea kuonyesha kuwa inaweza kuwa na ushindani dhidi ya Simba. Katika mechi za hivi karibuni, Simba ilikuwa ikitoka na ushindi mwembamba wa bao 1-0, ikiwemo michezo ya Februari 4, 2025, Desemba 22, 2025 na Aprili 26, 2026, kabla ya matokeo ya leo kutoa suluhu.

Mechi zingine zilizopigwa leo JKT Queens ikiwa Uwanja wa Mej Jenerali Isamuhyo imeshinda kwa mabao 3-0 yaliyowekwa kambani na Donisia Minja, Aliyah Fikiri na Bahati Kisanguzi.

Bunda Queens nayo imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Queens bao lililofungwa na Martha Chacha.