Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cannavaro: Mkomola ameanza kazi vizuri

Muktasari:

  • Mkomola aliyesajiliwa kutoka Serengeti Boys na ambaye amepewa jezi namba 31, ameanza kucheza mechi ya kwanza ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania Jumapili iliyopita tangu aliposajiliwa katika dirisha dog

NAHODHA wa Yanga, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema, Yohana Mkomola, ameanza vizuri na anaamini atakuwa msaada kwa timu.

Mkomola aliyesajiliwa kutoka Serengeti Boys na ambaye amepewa jezi namba 31, ameanza kucheza mechi ya kwanza ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania Jumapili iliyopita tangu aliposajiliwa katika dirisha dogo.

“Nafurahi kuona usajili mpya kwenye timu, nafikiri wanaweza kusaidia timu na uongozi umeliona hilo ndiyo maana wakasajili. Kwa upande wangu, Mkomola ameanza vizuri kwenye timu, namfahamu ni kijana mdogo na yuko vizuri,”alisema Cannavaro.

Kwa upande wa Mkomola alisema, anafurahi kuwepo ndani ya kikosi hicho, anaomba ushirikiano na wamuamini ili atafanye kazi nzuri.