Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bye bye Man United Ronaldo atua Real Madrid, aweka rekodi

Muktasari:

  • KATIKA toleo lililopita, mwandishi Luca Caioli aliyachambua mafanikio ya Messi ambaye tayari alianza kuonyesha dalili zote za kuwa mmoja wa mastaa wa dunia ingawa alipata pigo na kuumaliza kwa majanga msimu wa 2007/08. Sasa endelea…

KATIKA toleo lililopita, mwandishi Luca Caioli aliyachambua mafanikio ya Messi ambaye tayari alianza kuonyesha dalili zote za kuwa mmoja wa mastaa wa dunia ingawa alipata pigo na kuumaliza kwa majanga msimu wa 2007/08. Sasa endelea…

Kwa Messi ikawa huzuni baada ya Barcelona kumaliza msimu bila taji, mbele ya wengi alitoa kila dalili njema uwanjani kwa kipindi kirefu cha mwaka na uvumi ukaanza kuzagaa kwamba ndiye atakayekuwa mwanasoka bora duniani na ana nafasi ya kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia.

Hata hivyo Machi 4, 2008 alipata matatizo ya misuli ya paja katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Celtic na kujikuta akiwa nje ya uwanja mwezi mmoja na nusu. Alimaliza msimu na mabao 10 katika La Liga na sita katika Ligi ya Mabingwa.

2008/09

Mwaka uliofuata bahati ikahamia upande wake, Ronaldo na Messi wakakutana ana kwa ana, katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Roma Mei, 29, 2009. Barca wakatawala mchezo na kuilaza Man United mabao 2-0.

Pamoja na kulitetea taji la Ligi Kuu England na kuilaza Tottenham katika fainali ya Kombe la Carling, bado Ronaldo kwenye rekodi alikuwa aliyeipoteza siku yake ya mwisho akiwa na jezi ya Man United, ni kama aliiaga klabu hiyo.

Julai 6, 2009 Ronaldo alitambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Real Madrid mbele ya mashabiki 80,000 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, aliigharimu klabu hiyo Pauni 80 milioni na kuweka rekodi mpya ya dunia.

Kwa Messi ulikuwa mwaka wa furaha baada ya Barca kuwa timu ya kwanza Hispania kutwaa mataji matatu makubwa, La Liga, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Mfalme. Ni klabu tano tu Ulaya zilizo na rekodi ya kubeba mataji hayo matatu katika msimu mmoja. Mojawapo ya karibuni ni Man United.

Ni wakati ambao Messi alifunga mabao mengi kuliko wakati wowote katika historia yake kwenye soka la hadhi ya juu, katika La Liga alifunga mabao 23 na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji aliyefunga mabao mengi katika msimu wa La Liga akishika nafasi ya nne nyuma ya Diego Forlan, Eto’o na David Villa.

Mbali na hilo pia alikuwa na kumbukumbu ya bao la 5,000 la Barca katika historia ya klabu hiyo kwenye La Liga, alifunga bao hilo Februari Mosi, 2009 katika mechi dhidi ya Racing Santander, hilo lilikuwa bao lake la pili na kuiwezesha Barca kupata ushindi katika mechi hiyo.

Pia alikuwa na mabao mengine sita katika Kombe la Mfalme, ambako aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo licha ya kucheza dakika 452 tu katika michuano hiyo ambao ni wastani wa kila goli kufungwa baada ya dakika 75. Pamoja na mabao mengine mawili aliyoyafunga katika Spanish Super Cup.

Sambamba na hayo, Messi pia alifunga mabao tisa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumfanya awe mfungaji mwenye mabao mengi katika ligi hiyo. Tofauti na msimu uliopita, Messi wa msimu huu wa 2008/09 hakuandamwa na janga la majeraha katika mechi zote 51 alizocheza.

“Ulikuwa mwaka wa kipekee, nimeufurahia wote,’’ alisema Messi ambaye kubwa jingine alilovuna wakati huo ni kushika nafasi ya pili katika tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa dunia nyuma ya Ronaldo, lakini miezi 12 baadaye alimbwaga na kutwaa tuzo hiyo.

Itaendelea Jumamosi ijayo, usikose.