Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bunda Queens kambini wiki nane

BUNDA Pict

Muktasari:

  • Bunda Queens  ilimaliza katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kwenye michezo 22 walishinda sita, sare tatu , na kupoteza 13 ikikusanya pointi 18 baada ya kukatwa pointi tatu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kutokea changamoto ya kutocheza mchezo wao dhidi ya JKT Queens.

KOCHA wa Bunda Queens, Alley Ibrahim, amesema timu hiyo imejipanga kutumia wiki nane kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania kwa lengo la kurekebisha makosa ya msimu uliopita.

Alley amesema uamuzi wa kuingia kambini mapema umetokana na hitaji la kupata muda wa kutosha wa kuwaandaa wachezaji kimwili, kiufundi na kimkakati kabla ya msimu mpya haujaanza.

“Tumepata wiki nane za maandalizi na sababu ya kuingia mapema kambini ni kuhakikisha tunapata muda wa kutosha kujiandaa. Tunataka kutumia kipindi hiki kujenga timu vizuri zaidi,”  amesema Alley.

Kocha huyo amesema Bunda Queens haikuanza msimu uliopita kwa kiwango walichokitarajia, hali ambayo sasa imewafanya kuweka mkazo mkubwa kwenye maandalizi ili wasirudie makosa hayo msimu huu.

“Msimu uliopita hatukuwa na mwanzo mzuri, lakini sasa tunataka kujiboresha kwenye eneo la maandalizi. Tunataka kuanza vizuri na kuhakikisha timu inakuwa tayari kabla ya ligi kuanza,”€amesema.

Alley ameongeza kuwa muda wa wiki nane utawapa nafasi ya kuwafanyia kazi wachezaji kwa hatua tofauti, huku benchi la ufundi likiwa na nafasi ya kutambua mapungufu na kuyafanyia kazi kabla ya michezo ya ushindani.

Bunda Queens  ilimaliza katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kwenye michezo 22 walishinda sita, sare tatu , na kupoteza 13 ikikusanya pointi 18 baada ya kukatwa pointi tatu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kutokea changamoto ya kutocheza mchezo wao dhidi ya JKT Queens.