Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bondia Mgaya kuzikwa kesho Januari 2, Jeti Lumo

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Cheka amesema kuwa awali baba wa marehemu alitaka wazike leo kwa kuwa alitegemea angewahi kuingia nchini

Mweka hazina wa Chama cha mabondia wa ngumi za kulipwa nchini, Cosmas Cheka amesema kuwa bondia Hassan Mgaya sasa anatarajia kuzikwa kesho Januari 2, 2025 badala ya leo Jumatano kama ilivyotangazwa awali kutokana na kusubiriwa baba wa marehemu anayetarajia kuwasili leo kutokea DR Congo.

Cheka amesema kuwa awali baba wa marehemu alitaka wazike leo kwa kuwa alitegemea angewahi kuingia nchini lakini badala yake wamepanga kuzika kesho saa kumi jioni Jeti Lumo, Relini Dar es Salaam kumsubiri baba yake amb ambaye ataingia nchini leo

Hassan Mgaya, alifariki dunia Desemba 28, 2024 muda mchache baada ya kupewa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka Hospitali ya Mwananyamala ili akapatiwe matibabu baada ya kupigwa katika pambano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dunia Ndogo, Tandale jijini Dar es Salaam Desemba 27, 2024.

Inadaiwa chanzo cha bondia huyo kuwa katika hali mbaya kabla ya kufikwa na umauti ni baada kupigwa ngumi nyingi za kichwa katika raundi ya tano na mpinzani wake Paul Elias kabla ya kuanguka kisha kung’ata ulimi kuzama.

Baada ya tukio hilo, alipatiwa huduma ya kwanza na kurejea katika hali yake ya kawaida ambapo asubuhi ya Jumapili hali ilibadilika na kukimbizwa hospitali.

Bondia huyo anakuwa wa pili kufariki dunia hapa nchini kwa siku za karibuni baada ya pambano kufuatia mwezi uliopita mchezo wa ngumi kumpoteza bondia Abbasi Mselem aliyefariki kufuatiwa kupigwa katika pambano lake Zanzibar.