Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BMT yabariki kitabu cha soka

Muktasari:

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Halima Bushiri wakati akikabidhi vitabu 200 kwa kijana wa Mtanzania, Gambolii  Kimaya  ambaye ni mwandishi wa kitabu cha 'Boresha na endeleza kipaji chako cha soka umri kuanzia miaka 6 hadi 20'.

Dar es Salaam. Baraza Michezo Tanzania (BMT) limewashauri wazazi na walezi kuwanunulia vitabu vya soka watoto wenye vipaji ili kuendeleza vipaji vyao.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Halima Bushiri wakati akikabidhi vitabu 200 kwa kijana wa Mtanzania, Gambolii  Kimaya  ambaye ni mwandishi wa kitabu cha 'Boresha na endeleza kipaji chako cha soka umri kuanzia miaka 6 hadi 20'.
Halima alisema BMT imesaidia kuchapisha vitabu 200 kutokana na kufurahishwa na hatua ya kijana huyo wa kitanzania ya kuendeleza michezo nchini.
"BMT inampongeza kijana huyu kwa kazi nzuri aliyofanya kwa maendeleo ya michezo hapa nchini.
"Pia, tunatoa wito kwa wadau wengine wa michezo kumsaidia kuchapisha vitabu vingi ili elimu hii iwafikie watu wengi zaidi,"alisema Halima.
Naye Gambolii aliwashukuru BMT kwa kumsaidia kuchapisha vitabu 200 na kuwataka wadau wengine walioguswa kumsaidia kuchapisha vitabu vingine zaidi.
"Vitabu hivi vitawafikia walengwa waliokusudiwa hasa wachezaji na kitauzwa kwa kwa sh 5000,"alisema Gambolii ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Mwananchi.
Gambolii alipata elimu ya awali ya ukocha kwa kushirikiana na wanachuo wa kozi ya elimu ya michezo kwa vitendo kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam.