Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki KMC FC apania makubwa Championship

BEKI Pict

Muktasari:

  • Kabla ya mechi ya leo Jumapili nyumbani dhidi ya KenGold, KMC FC imeanza msimu wa 2026-2027, kwa kishindo, ikianza kwa kuichapa Mbuni FC ya jijini Arusha mabao 5-1, kisha ikaendeleza wimbi la ushindi kwa kuifunga Bigman FC ya Tanga 3-1.

BEKI wa kati wa KMC FC, Vintani Mtega amesema mwenendo mzuri wa timu hiyo hadi sasa unatoa matumaini ya kupambana zaidi kutokana na ushindani uliopo, jambo linaloongeza morali ya kukipambania kikosi hicho kirejee tena katika Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtega aliyejiunga na KMC FC msimu huu akitokea Mbeya Kwanza, amesema mwanzo mzuri wa kikosi hicho hadi sasa unatoa matumaini makubwa, japo wanahitaji kupambana zaidi ili waweze kufikia malengo waliyoweka pamoja.

"Malengo yangu kwa sasa ni kuipigania timu ili irudi tena Ligi Kuu Bara, kwa nafasi tuliyopo tunaweza kufanikisha hilo kutokana na ushirikiano tulionao kuanzia sisi wachezaji wenyewe, benchi la ufundi na viongozi kiujumla," amesema Mtega.

Nyota huyo aliyeanzia timu za vijana za Mbeya City kabla ya kujiunga na Mbeya Kwanza, amesema msimu huu umekuwa ni mgumu kutokana na ushindani mkubwa wa wapinzani wao, jambo linaloongeza ari kubwa ya kupambana katika kila mechi wanayoicheza.

KMC iliyoshuka daraja baada ya kumaliza mkiani mwa nafasi ya 16, katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026 na pointi tisa, imeanza vizuri katika Ligi ya Championship msimu wa 2026-2027, baada ya kushinda mechi zote mbili ilizocheza hadi sasa.

Kabla ya mechi ya leo Jumapili nyumbani dhidi ya KenGold, KMC FC imeanza msimu wa 2026-2027, kwa kishindo, ikianza kwa kuichapa Mbuni FC ya jijini Arusha mabao 5-1, kisha ikaendeleza wimbi la ushindi kwa kuifunga Bigman FC ya Tanga 3-1.