Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki kisiki Dante kitaeleweka tu Yanga

BEKI kisiki Andrew Vincent ‘Dante’ aliyemaliza mkataba na kikosi cha Yanga, anasubiri kujua hatima yake kwenye klabu hiyo kuanzia sasa.
Dante alisema kwamba hatma yake ndani ya Yanga itaeleweka baada ya kupita siku tano kuanzia kesho Jumatatu.
Beki huyo anayedabo na Beki Mkongwe, Kelvin Yondan, amekuwa akihusishwa kujiunga na Singida United kwa muda mrefu, lakini dili hilo lilichelewa baada ya kutulizwa na mabosi wa Yanga kwamba asiende popote kwani bado wanahitaji huduma yake.
Akizungumza na Mwanaspoti alisema kwamba ameshakutana mara kwa mara na viongozi wake wa zamani kuhusu kujua hatma yake ndani ya Yanga, lakini bado kumekuwa na ukimya wa muda mrefu kuhusu yeye.
“Nilikutana na bosi mmoja nilizungumza nae kuhusu masuala yangu ya nyuma kwanza akasema ataweka sawa, lakini bado haijawaha hivyo lakini nimeamua kuwapa muda wa siku tano ili nijue hatma yangu kama naendelea au naondoka kwasababu unaweza ukasubili na mambo yakawa tofauti,” alisema.