Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beimbaya azigonganisha KMC FC, JKT Queens

BEIMBAYA Pict

Muktasari:

  • Beimbaya aliyewahi kuifundisha pia Pan Africans, kwa sasa ameiongoza B19 FC ikishika nafasi ya 11 na pointi 30, baada ya kikosi hicho kushinda mechi nane, sare sita na kupoteza 12, ikifunga mabao 24 na kuruhusu 38.

KOCHA Mkuu wa B19 FC, Twaha Beimbaya amegeuka lulu sokoni baada ya KMC FC na JKT Queens kuanza mazungumzo rasmi ya kuipata saini yake msimu ujao, licha ya kubakisha mkataba wa mwaka mmoja na miezi sita katika kikosi hicho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Beimbaya amesema ni mapema sana kuzungumzia suala hilo kwa sababu bado kuna mechi zimebaki za kumalizia msimu, ambazo ni muhimu zaidi kwa kikosi hicho ambacho kinawania nafasi za kukwepa janga la kushuka daraja.

"Nilisaini mkataba wa miaka miwili na B19 na baada ya msimu huu kuisha nitakuwa nimebakisha mwaka mmoja na miezi sita, ni kweli kuna ofa za timu mbalimbali zilizoonyesha nia ya kunihitaji ingawa ni mapema kuziweka wazi," amesema Beimbaya.

Hata hivyo, licha ya kauli ya Beimbaya, taarifa ambazo Mwanaspoti ilizipata zinaeleza kocha huyo ameanza mazungumzo ya siri na uongozi wa KMC na JKT Queens kwa ajili ya msimu ujao, japo hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa hadi sasa.

Kocha huyo aliyeifundisha Kiluvya United kwa sasa Barberian, alipewa jukumu la kukiongoza kikosi cha B19 zamani Tanesco, baada ya uongozi wa timu hiyo kuachana na Babou Salim kwa makubaliano ya pande mbili kutokana na mwenendo usioridhisha.

Beimbaya aliyewahi kuifundisha pia Pan Africans, kwa sasa ameiongoza B19 FC ikishika nafasi ya 11 na pointi 30, baada ya kikosi hicho kushinda mechi nane, sare sita na kupoteza 12, ikifunga mabao 24 na kuruhusu 38.