Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker awatisha mastaa Simba

BARKER Pict


KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker amesema ushiriki wa timu hiyo katika michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026 utakuwa sehemu muhimu ya maandalizi kuelekea msimu mpya, akiamini mechi za ushindani zitawapa nafasi ya kutathmini maendeleo ya kikosi chake kabla ya kuanza kwa mashindano rasmi, huku akitaka vita kwa kila mchezaji kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza.


Simba ni miongoni mwa wawakilishi wa Tanzania Bara watakaoshiriki michuano hiyo pamoja na Singida Black Stars, huku mashindano yakitarajiwa kufanyika Kigali, Rwanda kuanzia Julai 24 hadi Agosti 7, yakizikutanisha baadhi ya klabu bora kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


Akizungumza kuhusu mashindano hayo, Barker amesema benchi lake la ufundi linaangalia zaidi namna ya kuijenga timu kuliko matokeo ya muda mfupi, akisisitiza kuwa kila mchezo utakuwa sehemu ya mchakato wa kuandaa kikosi kwa msimu mzima.

“Kagame Cup itatupa nafasi ya kuona tulipo kama timu, kuwaona wachezaji katika mazingira ya ushindani na kujua ni maeneo gani tunapaswa kuboresha kabla ya msimu kuanza,” amesema Barker.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini ambaye anatarajiwa kutua nchini leo, amesema michuano hiyo itatoa fursa kwa benchi la ufundi kuwaona wachezaji wapya wakizoeana na wenzao huku pia ikipewa nafasi ya kuendelea kujenga muunganiko wa kikosi baada ya mabadiliko yaliyofanyika kuelekea msimu wa 2026/27.

“Hatutakuwa tunatafuta ushindi pekee, bali tunataka kuona falsafa yetu ya uchezaji inaendelea kueleweka na wachezaji. Hiyo ndiyo faida kubwa ya kucheza mashindano ya aina hii kabla ya kuanza kwa ligi,” ameongeza.

Barker anaamini mechi za Kagame Cup zitamsaidia kupima utekelezaji wa mfumo wake wa uchezaji, kiwango cha utimamu wa wachezaji pamoja na ushindani ndani ya kikosi kabla ya Simba kuanza kampeni zake kwenye Ligi Kuu Bara, Kombe la CRDB Federation na michuano ya CAF.

Kocha huyo amesema ushindani wa kimataifa unaopatikana katika Kombe la Kagame ni tofauti na mechi za kirafiki, jambo ambalo litawasaidia wachezaji kuingia kwenye msimu mpya wakiwa tayari kukabiliana na presha ya mashindano.makubwa.

“Tunataka kila mchezaji apambanie nafasi yake. Hayo ndiyo mazingira tunayoyahitaji kwa sababu ushindani ndani ya kikosi ndiyo unaongeza ubora wa timu, hakuna mwenye namba yake kwa kuwa msimu uliopita alicheza, kila kitu kinaanza upya na mapambano ni mapya,” amesema Barker.

Kagame Cup ni miongoni mwa mashindano yenye historia ndefu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, yakitumika kama sehemu ya kuzipima klabu kabla ya kuanza kwa misimu ya ndani na mashindano ya CAF.

Historia ya mashindano hayo inaanza mwaka 1926 kupitia michuano iliyojulikana kama Gossage Cup ambayo mwanzoni ilihusisha Kenya na Uganda pekee. Tanganyika ilijiunga mwaka 1945, kabla ya Zanzibar kushiriki mwaka 1949 na kufanya mashindano hayo kupanuka zaidi katika ukanda huo.

Ratiba inaonyesha Simba ipo kundi B na  Singida Black Stars (mabingwa watetezi), Jamus SC (Sudan Kusini) na Mogadishu City ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Kagame Cup, ikiwa imetwaa ubingwa mara sita, ikizipiku klabu nyingine zote za ukanda huo.

Wekundu wa Msimbazi walitwaa mataji hayo mwaka 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002, rekodi inayowafanya waingie kwenye michuano ya mwaka huu wakiwa na hadhi ya timu yenye historia kubwa zaidi kwenye michuano hiyo.