Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker aanza mpango wa ubingwa


SIMBA imeanza msimu wa Ligi Kuu Bara kwa kasi ya kutisha, ikionyesha kuwa safari hii imejipanga kupambana kwa nguvu kuwania ubingwa, huku ushindi dhidi ya wapinzani wakubwa ukiendelea kuipa nafasi ya kujiamini katika mbio hizo.


Wekundu hao wa Msimbazi wamecheza mechi nane za ligi na kushinda zote, wakikusanya pointi 24, kufunga mabao 19 na kuruhusu manne pekee, rekodi inayowaweka kileleni mwa msimamo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Simba Steven Barker alisema mwenendo huo ni hatua kubwa katika safari ya kuwania ubingwa, lakini akasisitiza kuwa bado kuna kazi ya kufanya kutokana na mechi nyingi zilizosalia, hasa za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

“Ni hatua kubwa kwetu, lakini bado tuna mechi nyingi za kucheza. Tunachotakiwa ni kuendelea kupambana na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika kila mchezo,” alisema Barker.

Alisema siri ya mafanikio hayo ni kujitoa kwa wachezaji ndiko kunakoifanya timu hiyo kuendelea kupata matokeo mazuri, akieleza kuwa wameamua kupambana kwa ajili ya klabu yao.

“Nafikiri kinachotusaidia ni namna wachezaji walivyoamua kujitoa kwa ajili ya timu. Wanaonyesha dhamira ya kupambana na kufanya vizuri, lakini tunapaswa kuendelea kuwa na umakini kwa sababu lengo letu ni ubingwa,” amesema.

Simba bado inahitaji kuendeleza kasi hiyo katika mechi 22 zilizosalia ili kuhakikisha haidondoshi alama hata moja ili kujihakikishia ubingwa mbele ya mabingwa watetezi, Yanga.

Simba haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara tangu mara ya mwisho walipobeba taji hilo katika msimu wa 2020–2021. Baada ya kutawala soka la nchini kwa kutwaa ubingwa mara nne mfululizo kuanzia msimu wa 2017–2018, klabu hiyo imeshuhudia watani wao wa jadi, Yanga, wakitwaa vikombe vyote vya ligi kuu vilivyofuata, jambo linalofanya sasa kukaa misimu mitano mfululizo (2021–22, 2022–23, 2023–24, 2024–25, na 2025–26) bila kutwaa taji hilo kubwa nchini.

Mchezo ujao wa kimataifa wa Simba itakuwa dhidi ya klabu ya 15 de Agosto kutoka Guinea ya Ikweta katika hatua ya pili ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 17, 2026, saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kutokana na wapinzani wao kuchagua kutumia uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani, Simba itapata faida ya kucheza mechi zote mbili ya mkondo wa kwanza Oktoba 17, 2026 na ya marudiano Oktoba 24, 2026, hapa hapa nchini kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.