Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baraza awatuliza mashabiki Pamba Jiji

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hizo tatu, Pamba Jiji ilianza kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Dodoma Jiji, ikapoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Simba, matokeo ambayo sawa na iliyopata kwa Azam, jambo ambalo Baraza amesema siyo matokeo mazuri kwao na kusisitiza wanahitaji kupata ushindi.

KOCHA wa Pamba Jiji, Francis Baraza amesema japokuwa wameanza msimu kwa kukosa matokeo ya ushindi wakivuna alama moja kati ya mechi tatu walizocheza, anaamini kikosi chake kina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri michezo iliyopo mbele, hivyo ni suala la muda kusubiri na kuona.

Katika mechi hizo tatu, Pamba Jiji ilianza kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Dodoma Jiji, ikapoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Simba, matokeo ambayo sawa na iliyopata kwa Azam, jambo ambalo Baraza amesema siyo matokeo mazuri kwao na kusisitiza wanahitaji kupata ushindi.

“Ingawa hakuna timu nyepesi Ligi Kuu Bara, lakini Simba na Azam zimetupa chalenji kubwa na dakika 90 ziliamua pointi tatu ziende kwao, lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya mechi zilizopo mbele yetu,” amesema Baraza na kuongeza;

“Naamini tutafanya vizuri katika mechi zilizopo mbele yetu, natambua mwanzo wa ligi siyo mwepesi kwani kila timu inakuwa imejipanga kuanza na ushindi pia kuna mambo ya maandalizi, hivyo kadri muda unavyokwenda ndivyo ushindani unavyozidi kuwa mgumu.”

Msimu uliopita Pamba Jiji ilimaliza nafasi ya saba, katika mechi 30, ilishinda tisa, sare tisa, ilifungwa 12, ilivuna pointi 36, jambo ambalo Baraza anatamani kumaliza nafasi za juu zaidi.

“Tunatamani kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita, ingawa natambua ligi ni ngumu lakini tupo tayari kwa ushindani.”

Baada ya kumalizana na Azam, Pamba Jiji inakwenda kukutana na Yanga, mechi itakayopigwa Agosti 28, 2026 kwenye Uwanja wa KMC, ambapo Baraza alisisitiza haitakuwa rahisi lakini wamejipanga kuhakikisha wanapambania pointi tatu.