Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yaishusha Yanga ikiichapa Pamba Jiji

AZAM Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Azam ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya 24 kupitia Mkongomani, Henoc Molia aliyemalizia pasi iliyopigwa na Idd Seleman 'Nado'.

AZAM FC imesogea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi saba ikiishusha Yanga yenye pointi sita, baada ya leo Agosti 23, 2026 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Azam ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya 24 kupitia Mkongomani, Henoc Molia aliyemalizia pasi iliyopigwa na Idd Seleman 'Nado'.

Bao hilo la Molia aliyejiunga na Azam FC, Julai 18, 2026, akitokea FC Saint-Eloi Lupopo ya kwao DR Congo, lilidumu hadi dakika 45+2, baada ya Pamba Jiji kusawazisha kupitia beki wa kati raia wa Nigeria, Nonyem Okorocha.

AZA 02

Okorocha aliyejiunga na Pamba Jiji msimu huu akitokea Mlandege FC ya Zanzibar, alifunga bao hilo baada ya beki wa Azam FC, Twalibu Nuru kuupiga mpira kichwa akiwa anaokoa krosi ya Salehe Karabaka na nyota huyo kuunganisha pia kwa kichwa.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kuendelea kulishambulia lango la Pamba Jiji na dakika ya 62, kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho, Abdul Suleiman 'Sopu' aliifungia kwa penalti na kuihakikishia timu hiyo pointi tatu.

Sopu alifunga bao hilo kwa penalti baada ya Idd Seleman 'Nado' kufanyiwa madhambi eneo la hatari na beki wa kulia wa Pamba Jiji, Hassan Kibailo na kuifunga kwa ustadi mzuri na kuipatia timu hiyo ushindi wa pili mfululizo wa Ligi Kuu.

AZA 01

Bao hilo la Sopu ambalo limedumu hadi dakika 90 za mechi hiyo, limemfanya nyota huyo kufikisha mabao matatu ya Ligi Kuu Bara msimu huu, akiwa sawa na mshambuliaji wa Geita Gold, Mzambia Obrey Chirwa ambao kwa sasa ndio wanaoongoza.

Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa Azam FC katika Ligi Kuu katika mechi tatu ilizocheza msimu huu, baada ya Agosti 20, 2026, kuifunga pia TRA United mabao 2-1, kufuatia kuanzia msimu kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, Agosti 15, 2026.

Kwa upande wa Pamba Jiji, kichapo hiki ni cha pili mfululizo baada ya Agosti 19, 2026, kuchapwa pia mabao 2-1 dhidi ya Simba, ikicheza nyumbani, huku ikianza msimu huu kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Dodoma Jiji, Agosti 14, 2026.

Matokeo ya leo yanaifanya Azam FC kufikisha pointi saba ikiwa nafasi ya pili ikicheza mechi tatu na kuishusha Yanga yenye pointi sita iliyocheza mechi mbili, huku kwa upande wa Pamba Jiji ikiendelea kushika nafasi ya 12 na pointi moja.