Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Banda apewa miaka miwili Dodoma Jiji

BANDA Pict

Muktasari:

  • Banda ni mmoja kati ya wachezaji wenye kiwango cha juu kwenye kikosi cha Dodoma lakini akiwa na uzoefu wa kutosha baada ya kucheza ligi kuu kwa muda mrefu akiwa aliwahi pia kuzitumikia Simba na Coastal Union kwa vipindi tofauti.

BEKI wa kati wa Dodoma Jiji, Abdi Banda ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikikusanya pointi 35.

Banda ni mmoja kati ya wachezaji wenye kiwango cha juu kwenye kikosi cha Dodoma lakini akiwa na uzoefu wa kutosha baada ya kucheza ligi kuu kwa muda mrefu akiwa aliwahi pia kuzitumikia Simba na Coastal Union kwa vipindi tofauti.

Akizungumza na Mwanaspoti, msimamizi wa mchezaji huyo, Fadhili Sizya amesema Banda ameamua kusalia Dodoma Jiji licha ya kupata ofa kutoka Morocco na sehemu nyingine.

Sizya amesema Banda alikuwa amepokea ofa kutoka moja ya klabu za Morocco baada ya kumaliza msimu uliopita kwa  kiwango kizuri akiwa Dodoma Jiji.

Hata hivyo, mazungumzo hayo yalikwama kutokana na baadhi ya vipengele vya mkataba kushindwa kukidhi matarajio yake, jambo lililomfanya aamue kubaki Tanzania. Inadaiwa kuwa beki huyo alifanya uamuzi huo ili kupata utulivu na familia yake akiamini bado ana nafasi ya kuendelea kuisaidia timu msimu ujao.

“Amesaini miaka miwili lakini alikuwa  na ofa Morocco na timu nyingine ila kulikuwa na masharti ambayo hajakubaliana nayo kwa hiyo aliona bora zaidi abaki Tanzania kutimiza malengo ya timu,” amesema Sizya.

Mbali na kuwa na uzoefu kwenye ligi pia beki huyo wa kati amewahi kutumika kwenye timu kadhaa nchini Afrika Kusini, akiwa Afrika Kusini aliitumikia Baroka FC (2017/19), ambapo alidumu kwa misimu miwili na kucheza mechi 41 za ligi akifunga mabao manne, kabla ya kujiunga na Highlands Park (2019/20).

Baadaye aliitumikia TS Galaxy, akarejea Tanzania kuichezea Mtibwa Sugar, kisha akarudi Afrika Kusini akikipiga Chippa United na baadaye Richards Bay kabla ya kurejea nyumbani na kusaini Dodoma Jiji Januari 2025.  Uzoefu huo ndiyo unaomfanya kuwa mmoja wa viongozi muhimu ndani ya kikosi cha Dodoma Jiji, ambacho kitaendelea kunufaika na huduma yake kwa misimu miwili ijayo.