Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Badru aichambua Stars akiwataja vijana

Muktasari:

  • Badru ametoa kauli hiyo baada ya Taifa Stars kuanza vibaya kampeni ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), baada ya kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau.

KOCHA wa timu ya vijana ya Yanga, Mohamed Badru, amesema Tanzania bado ina safari ndefu katika kujenga Taifa Stars yenye uwezo wa kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa ya Afrika, akielekeza matumaini zaidi kwenye programu za timu za vijana za chini ya miaka 20 na 23.

Badru ametoa kauli hiyo baada ya Taifa Stars kuanza vibaya kampeni ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), baada ya kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau.

Kocha huyo amesema licha ya matokeo hayo, haoni Tanzania ikiwa mbali sana na kufikia kiwango kinachohitajika, lakini akasisitiza kuwa mabadiliko makubwa hayawezi kufanyika kwa muda mfupi bila kuweka mkakati wa muda mrefu wa kuzalisha na kuwaendeleza wachezaji.

“Kwa maoni yangu, ninachokiona ni kwamba hatuko mbali, hatuko pabaya sana, lakini bado tuna safari ndefu kubwa,” amesema Badru.

Kocha huyo wa zamani wa Gwambina na Mtibwa Sugar, ameongeza kuwa kwa kipindi hiki, Tanzania inapaswa kuwa na matarajio yanayolingana na hali halisi ya timu huku akisisitiza jukumu kubwa ni kuhakikisha Taifa Stars inaendelea kushiriki katika mashindano makubwa kama AFCON, wakati mipango ya muda mrefu ikiendelea kujengwa chini.

“Safari hii itakuja kutatuliwa kupitia mradi wa U-20 na U-23. Hiyo ndiyo picha ilivyo. Hatuwezi kuitatua kwa kipindi hiki,” amesema.

Badru amesema timu ya wakubwa haiwezi kubadilishwa kwa muda mfupi na kugeuka kuwa timu inayotawala soka la Afrika, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuijenga huku nguvu kubwa ikiwekwa kwenye mifumo ya vijana ambao ndio msingi wa Taifa Stars ya baadaye.

Kwa mujibu wa Badru, kinachotia matumaini ni kwamba Tanzania tayari imeanza kuonyesha dalili nzuri katika ngazi za vijana, akitaja timu za Taifa za chini ya miaka 17, 20 na 23 kama sehemu muhimu ya mabadiliko ya soka nchini.

Badru ameeleza kuwa timu hizo za vijana zimeanza kucheza kwa mtindo unaoendana zaidi na mahitaji ya soka la kisasa, tofauti na changamoto zinazoweza kuonekana katika timu ya wakubwa.