Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI wa Kenya ajipanga upya

AZIZ Pict

Muktasari:

  • Aziz KI amejiunga na Mombasa United inayoshiriki Ligi Kuu Kenya kwa mkopo wa msimu mzima wa 2026-2027, ambapo nyota huyo ameungana na kikosi hicho kinachofundishwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin ‘Master Lecturer’.

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Mzee Hassan Mzee ‘Aziz KI’ amesema ni wakati mzuri kwake wa kupata changamoto sehemu nyingine mpya baada ya kukamilisha uhamisho wa msimu kujiunga na Mombasa United ya Kenya.

Aziz KI amejiunga na Mombasa United inayoshiriki Ligi Kuu Kenya kwa mkopo wa msimu mzima wa 2026-2027, ambapo nyota huyo ameungana na kikosi hicho kinachofundishwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin ‘Master Lecturer’.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mzee amesema kujiunga na timu hiyo ni fursa nyingine nzuri katika maisha yake ya kubadilisha mazingira na Ligi nyingine, huku akijivunia kufanya kazi na Kocha Mkuu, Abdihamid Moallin wanaofahamiana naye vizuri. “Nimekuja Kenya kwa ajili ya kuonyesha kipaji nilichokuwa nacho, hii ni fursa nyingine kwangu ya kupata changamoto mpya ya kunikuza maishani mwangu, lengo ni kufanya vizuri katika kipindi chote cha msimu wa 2026-2027,” amesema Mzee.

AZIZ 01

Nyota huyo amesema ushindani wa Ligi Kuu Bara hauna tofauti kubwa na Kenya, japo jambo la muhimu ni kuendelea kupambana kwa ajili ya kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza, ili kuendeleza kiwango kizuri.

Nyota huyo anayefananishwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI, alijiunga na Azam FC katika dirisha dogo la Januari 2026, akitokea KMKM ya Zanzibar, baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia.

Licha ya ushindani wa nafasi ya kucheza mara kwa mara, nyota huyo alichangia bao moja tu la Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026.