Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yarudi tena kwa winga

SILLAH Pict

Muktasari:

  • Unaposoma taarifa hii tambua kwamba winga wa zamani wa Azam Djibril Silla wakati wowote anarejea klabuni hapo baada ya kuwa na kwa msimu mmoja uliopita, akienda kuzitumikia klabu mbili tofauti ndani ya Afrika.

HAWA Azam wameamua kujiamulia mambo na sasa imemrudisha tena winga wake mwingine aliyekuwa anawatungua Simba na Yanga akija kukipa nguvu kubwa kikosi chao kwenye hesabu zilezile za kuutaka ubingwa msimu ujao.

Unaposoma taarifa hii tambua kwamba winga wa zamani wa Azam Djibril Silla wakati wowote anarejea klabuni hapo baada ya kuwa na kwa msimu mmoja uliopita, akienda kuzitumikia klabu mbili tofauti ndani ya Afrika.

Azam inamrudisha Silla akiwa winga wake wa pili kufanya hivyo akitanguliwa na Kipre Junior ambaye tayari ameshatambulishwa akirudi kuja kuirudishia makali timu hiyo inayotaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kufika mbali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Silla raia wa Gambia, baada ya kuondoka Azam akiwa mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake, alijiunga na ES Setif ya Algeria, akiitumikia kwa miezi sita tu kisha kuvunjiwa mkataba na kujiunga na Al Ahly ya Libya ambako nako amecheza kwa nusu msimu pekee.

Taarifa kutoka ndani ya Azam  ni kwamba Silla anarudi klabuni hapo ikiwa ni kuendelea kuimariosha timu hiyo katika viungo wa pembeni,akibebwa na rekodi zake kabla ya kuondoka kwa matajiri hao wa Chamazi.

“Tunamrudisha Silla kweli, ni kijana wetu alifanya kazi nzuri kabla ya kuondoka, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini alikutana na bahati mbaya alipoondoka na kwenda kucheza nje ya Azam,”amesema bosi huyo.

“Wakati anataka kuondoka tulitaka kumbakisha lakini alituomba kwamba aende akajaribu kucheza nje tukamfungulia milango, amesema kama akikwama atarudi hapa na amefanya hivyo kweli, atarudi kwenye makali yake.

Silla kabla ya kuondoka Azam msimu wa juzi alifanikiwa kufunga mabao 11 akiwa na asisti mbili akizidiwa na Feisal aliyekuwa na asisti 13

Azam imeshasajili mawinga watatu wa kigeni wakiwemo Kipre, Silla na Mkongomani Enock Molia ambaye anatua kwa matajiri hao akitokea FC Lupopo, akinunuliwa kwa fedha ndefu.