Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yaweka rekodi CAF

CHAMAZI Pict

Muktasari:

  • Azam iliyoingia kwenye mchezo huo ikihitaji ushindi au suluhu ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele, ilifanya kazi yake mbele ya mashabiki waliojaa uwanjani kwa kupata bao moja lililotosha kuamua hatima ya timu hizo mbili.

BAO la dakika ya 63 la winga Idd Nado limeipa Azam FC rekodi mpya ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu wa pili mfululizo, baada ya kuizamisha Zed FC ya Misri kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Azam iliyoingia kwenye mchezo huo ikihitaji ushindi au suluhu ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele, ilifanya kazi yake mbele ya mashabiki waliojaa uwanjani kwa kupata bao moja lililotosha kuamua hatima ya timu hizo mbili.

Matokeo hayo yaliifanya timu hiyo ya Chamazi kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa ugenini kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na timu hiyo kuweka rekodi ya kuwa ya kwanza nchini nje ya Simba na Yanga kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili.

CHAMA 01

Nado ndiye aliyeibeba Azam katika michezo hiyo miwili, akifunga mabao yote mawili yaliyoihakikishia timu hiyo nafasi ya kucheza hatua ya makundi.

Kwenye mchezo wa kwanza nchini Misri, winga huyo alionyesha uwezo wake kwa kufunga bao kwa shuti kali baada ya kumalizia pasi ya beki wa kulia, Pascal Msindo.

Nado alifanya tena kile alichokifanya ugenini, akitumia nafasi aliyopata dakika ya 63 kuandika bao pekee la mchezo, alimalizia pasi ya Abdul Suleiman ‘Sopu’ aliyepokea krosi iliyochongwa na Msindo.

CHAMA 02

Kufuzu huko kunaifanya Azam kuendelea kuweka historia katika mashindano hayo ya Afrika, ikiwa ni mara ya pili mfululizo kufika hatua ya makundi. Msimu uliopita, timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi lake ikiwa na pointi tisa.

Kufuzu kwa Azam kunaongeza idadi ya timu za Tanzania zilizofikia hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika katika msimu huu, baada ya Yanga kutinga hatua hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Simba na Singida BS ambazo zinacheza leo nazo zikiwa na nafasi ya kufanya hivyo.

CHAMA 03

Kama Simba na Singida nazo zitafuzu, basi Tanzania itaweka rekodi mpya pia ya timu zake nne kutinga hatua ya makundi kwa mwaka wa pili mfululizo.