Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yakomaa kibishi Misri ikilazimisha sare na ZED FC

AZAM Pict

Muktasari:

  • Azam inasaka kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita.

Azam FC imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho msimu huu baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini na ZED FC ya Misri, leo Ijumaa, Oktoba 16, 2026.

ZED FC ndio imekuwa ya kwanza kupata bao katika mchezo kupitia kwa Mahmoud Shokry katika dakika ya 45.

Shokry amefunga bao hilo kwa shuti kali la mguu wa kulia akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aishi Manula baada ya kona iliyochongwa na timu hiyo ya Misri.

AZA 01

Bao hilo lilidumu hadi filimbi ya kumaliza kipindi cha kwanza ilipopulizwa.

Kipindi cha pili kilionekana kuwa na neema kwa Azam FC ambayo ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Iddy Seleman ‘Nado’ katika dakika ya 58.

Nado alifunga bao hilo kwa shuti kali la mguu wa kulia akimalizia pasi ya Pascal Msindo.

Matokeo yanaifanya Azam FC ihitaji ushindi wa aina yoyote katika mechi ya marudiano nyumbani mwishoni mwa wiki ijayo ili itinge hatua ya makundi.

Azam pia inaweza kusonga mbele ikiwa mechi hiyo ya marudiano itakayochezwa katika Uwanja wa Azam Complex, itamalizika kwa sare ya bila kufungana.

AZA 02

Kama itamalizika kwa sare ya bao 1-1, mshindi atapatikana kwa mikwaju ya penalti.

Mambo yatakuwa magumu kwa Azam FC ikiwa ZED FC itapata ushindi au kutoka sare kwenye mechi hiyo ya marudiano.

Azam inasaka kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo.

Mara ya kwanza ilikuwa ni msimu uliopita ambapo ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi lake baada ya kukusanya pointi tisa.