Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arajiga kusimama kati Dabi ya Kariakoo

Muktasari:

  • Mchezo wa mwisho wa Dabi ya Kariakoo ambao ulichezeshwa na Ahmed Arajiga ulikuwa ni Agosti 12, 2026 ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara, ametangazwa kuwa refa wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo baina ya Simba na Yanga utakaochezwa Jumamosi, Oktoba 10, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Uteuzi wa Arajiga umefanyika ikiwa ni miezi miwili tangu alipochezesha mechi ya Ngao ya Jamii baina ya timu hizo katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Agosti 12, 2026.

Katika mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeonyesha kwamba Arajiga katika mechi ya kesho Jumamosi, atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga kama Msaidizi namba moja na Alli Ramadhan kutoka Zanzibar atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.

ARA 01

Mwamuzi wa akiba atakuwa ni Alex Pancras kutoka Dar es Salaam.

TPLB imemteua Cyprian Kwiyava kutoka Iringa kuwa Kamishna wa Mchezo na Mratibu wa Mechi ni Mohamed Kaluma wa Dar es Salaam.

Timu hizo zinakutana huku zikiwa na idadi sawa ya pointi baada ya kila moja kucheza mechi sita za Ligi Kuu msimuu zikishinda zote.

Yanga iko juu ya msimamo kwa utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa huku Simba ikiwa katika nafasi ya pili japo kila moja ina pointi 18.

Yanga imefunga mabao 16 na kufungwa mawili huku Simba ikifunga mabao 11 na kufungwa mawili.