Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anachokipigania mbisa hiki hapa

Muktasari:

  • Msimu uliopita, Mbisa aliweka rekodi nzuri kwa kuwa miongoni mwa makipa wazawa waliofanya vizuri zaidi, baada ya kumaliza msimu akiwa na idadi nzuri ya clean sheets wakati akiitumikia Tanzania Prisons.

GOLIKIPA wa Dodoma Jiji, Mussa Mbisa, baada ya kufikisha clean sheets sita, anaamini ana nafasi ya kumaliza msimu huu akiwa na idadi kubwa zaidi ya mechi alizomaliza bila kuruhusu bao ikilinganishwa na alizofikisha msimu uliopita.

Msimu uliopita, Mbisa aliweka rekodi nzuri kwa kuwa miongoni mwa makipa wazawa waliofanya vizuri zaidi, baada ya kumaliza msimu akiwa na idadi nzuri ya clean sheets wakati akiitumikia Tanzania Prisons.

Ingawa anakiri kuwa ni vigumu kuibuka kinara wa clean sheets wa msimu huu mbele ya makipa wa Simba na Yanga, kama ilivyowahi kutokea kwa Ley Matampi msimu wa 2023/24 akiwa na Coastal Union ya Tanga, ambapo alimaliza akiwa na clean sheets 15 huku Diarra wa Yanga akifuatia kwa 14, Mbisa anaamini anaweza kufikisha idadi kubwa zaidi ya aliyonayo sasa.

"Kinachozibeba Simba na Yanga ni kwamba tumetofautiana kwa kiwango kikubwa katika ubora wa wachezaji mmoja mmoja. Hata hivyo, kuna makipa wanaofanya mambo makubwa nje ya timu hizo," alisema Mbisa na kuongeza:

"Mfano, msimu wa 2024/25, Patrick Munthali wa Mashujaa alikuwa na clean sheets 12 na kumaliza nafasi ya tatu. Nafasi ya kwanza ilikwenda kwa aliyekuwa golikipa wa Simba, Moussa Camara, aliyekuwa na 19, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Diarra wa Yanga aliyekuwa na 17.

"Jambo ambalo ninaamini ninaweza kulifikia ni kumaliza msimu huu nikiwa na clean sheets saba au zaidi, ikilinganishwa na saba nilizokuwa nazo msimu uliopita. Ikitokea nikapata tuzo ya kipa bora, itakuwa vizuri, lakini kikubwa ni kupambana na kuendelea kuonyesha kiwango bora."