Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tisa wana kazi yao Yanga, wamo Morrison, Aziz Ki

Tisa wana kazi yao Yanga

USAJILI uliofanywa na Yanga katika dirisha la usajili umeifanya iwe na silaha tisa ambazo zinaweza kuipa faida kubwa katika mbio za ubingwa mbele ya washindani wao wakuu Simba na Azam.

Katika kikosi cha wachezaji 30 ambao timu hizo kila moja itawasajili kwa ajili ya Ligi Kuu na michuano mingine msimu ujao, Yanga imepiga bao la kisigino kwa kuwa na nyota tisa wenye uwezo wa kucheza katika nafasi nyingi tofauti uwanjani zaidi na ilivyo kwa Azam na Simba..

Wachezaji hao wa Yanga wenye uwezo wa kucheza kwa ufanisi wa hali ya juu nafasi nyingi tofauti uwanjani ni Kibwana Shomari, Dickson Job, Yannick Bangala, Aziz Ki, Lazarous Kambole, Salum Abubakar, Feisal Salum, Bernard Morrison na Farid Musa.

Licha ya kila nafasi katika kikosi chake kuwa na wachezaji wawili au watatu wanaomudu vyema kuicheza, uwepo wa nyota hao viraka unaifanya Yanga kuwa na uhakika wa kumudu msimu mzima na kushiriki vyema katika michuano mingi tofauti hata ikitokea baadhi yao kuwa majeruhi na wengine kutokuwa na kiwango kizuri kwa wakati husika.

Uwepo wa Job, Kibwana na Bangala wanaoweza kucheza katika nafasi tofauti za ulinzi kwa ufanisi nmkubwa, unaipa Yanga jeuri katika msimu ujao wa kuwa na ukuta imara hata pale inapotokea mmoja kati ya mabeki wengine, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Ibrahim Baka, Djuma Shaban na David Bryson anapokosekana.

Wakati Job akimudu kucheza nafasi ya beki wa kati, beki wa kulia na kiungo mkabaji, Bangala anaweza kucheza nafasi zote uwanjani isipokuwa kipa huku Kibwana akionyesha kumudu nafasi ya beki wa kulia, kushoto na hata winga.

Ukimuondoa Bangala ambaye mara kwa mara amekuwa akitumika kama kiungo, viungo wengine wa Yanga wenye kuipa wigo mpana wa uteuzi wa kikosi benchi lao la ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi iwapo baadhi ya wachezaji watakosekana ni Feisal, Aziz Ki, Farid Musa na Sure Boy.

Feisal na Sure Boy kila mmoja anaweza kucheza nafasi ya kiungo namba sita, nane, winga na namba 10 wakati Ki anamudu nafasi ya winga, kiungo mshambuliaji na hata kucheza kama mshambuliaji wa kati.

Farid ameonyesha uwezo mkubwa wa kucheza kama beki na winga wa kushoto, kiungo namba 10, pia anaweza kucheza hata namba nane.

Katika ushambuliaji, Yanga ina Morrison na Kambole ambao kila mmoja anamudu kucheza nafasi ya winga, mshambuliaji wa kati na pia namba 10.

Wakati Yanga ikiwa hivyo, Simba yenyewe ina nyota saba viraka ambao ni Kibu Denis, Moses Phiri, Shomari Kapombe, Nassoro Kapama, Jimmyson Mwanuke na Mzamiru Yassin.

Kapama anamudu kucheza nafasi zote uwanjani, Nyoni, Kapombe na Mzamiru wanamudu kucheza zile za beki na kiungo wakati Mwanuke anamudu beki na wingi ya kulia.

Upande wa Phiri na Kibu kila mmoja anaweza kucheza katika nafasi ya mshambuliaji wa kati na pia winga.

Kama ilivyo kwa Simba, Azam nayo ina wachezjai saba viraka ambao ni Nathaniel Chilambo, Daniel Amoah, Lusajo Mwaikenda, Kenneth Muguna, Prince Dube, Ibrahim Ajibu na James Akaminko.

Amoah na Mwaikenda wanamudu kucheza vyema nafasi zote za ulinzi isipokuwa ile ya kipa wakati Chilambo anaweza kucheza beki wa kulia na kushoto wakati huo Akaminko akiwa ana uwezo wa kucheza nafasi zote za ndani.

Muguna anaweza kucheza nafasi ya kiungo wa ulinzi, ushambuliaji na beki wa kati huku Ajibu akiweza kucheza kama mshambuliaji wa kati na kiungo mshambuliaji na kwa upande wa Dube, anafiti akipangwa namba tisa, namba 10 na winga.