Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge afurahishwa na kiwango cha Simba, Yanga Singida CAF

Muktasari:

  • Simba Jumapili iliyopita ilikuwa nchini Malawi ikivaana na Mighty Wanderers na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, huku Yanga ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Gaborone ya Botswana na Singida BS ikiichapa mabao 7-1 Al Ghazala ya Sudan ya Kusini.

KOCHA Mkuu wa Azam Florent Ibenge amesema amefurahishwa na kiwango ambacho kimeonyeshwa na timu za Tanzania kwenye michuano ya CAF.

Simba Jumapili iliyopita ilikuwa nchini Malawi ikivaana na Mighty Wanderers na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, huku Yanga ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Gaborone ya Botswana na Singida BS ikiichapa mabao 7-1 Al Ghazala ya Sudan ya Kusini.

Simba na Yanga zilikuwa zikicheza michezo ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Singida ikicheza hatua hiyo kwenye Kombe la Shirikisho na kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufuzu hatua inayofuata kutokana na ushindi huo mnono zaidi iliyoupata.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam juzi, Ibenge raia wa DR Congo ambaye timu yake itaanzia hatua inayofuata kutokana na matokeo yao mazuri kwenye michuano hiyo msimu uliopita, alisema alizifuatilia timu zote na kuona kila moja ilionyesha kiwango kizuri sana na hata matokeo waliyopata ni mazuri.

“Nimefurahishwa na matokeo ya Simba, Yanga na hata Singida BS kwenye michuano ya CAF ya wikiendi iliyopita, kila timu ilionyesha kiwango kizuri na matokeo waliyopata yanaridhisha, sina shaka sana.

‘’Tukiwa kwenye michuano ya CAF inabidi kila mmoja kwenye hii nchi amuunge mkono mwenzake, hii ndiyo njia ya kuleta maendeleo ya soka hapa nchini, lakini tukirudi kwenye ligi kila mmoja apambane kivyake kuhakikisha timu yake inapata ushindi,’’ alisema Ibenge kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya DR Congo.

Ibenge ambaye alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na RS Berkane msimu wa 2021–22 ni kati ya makocha wenye mafanikio makubwa zaidi kwenye Ligi Kuu Bara, huku msimu uliopita akiiwezesha Azam kufika hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo na kufanikiwa kukusanya pointi tisa kwenye hatua hiyo.