Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Hat-Trick’ zatwala Kombe La Dunia, Hispania ikiichapa Fiji 15-0

SPAIN Pict

Muktasari:

  • Kipigo hicho kimeifanya Hispania kujihakikishia tiketi ya kufuzu hatua ya 32 bora, ikiwa na Rafael Cruz kama shujaa wa mchezo baada ya kufunga mabao matano.

'HAT-TRICK' zimeendelea kuwa gumzo katika mechi za pili za hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la FIFA U-17 Qatar 2026, huku Hispania ikiweka rekodi ya ushindi mnono baada ya kuichakaza Fiji mabao 15-0 katika mchezo wa Kundi H uliopigwa Uwanja wa Aspire Zone 4.

Kipigo hicho kimeifanya Hispania kujihakikishia tiketi ya kufuzu hatua ya 32 bora, ikiwa na Rafael Cruz kama shujaa wa mchezo baada ya kufunga mabao matano.

Hispania imekuwa timu pekee katika mechi hizo kufunga hat-trick tatu ndani ya mechi moja, zikifungwa na Rafael Cruz aliyepachika matano dakika ya 5, 10, 21, 57 na 65, Roberto Tomas aliyefunga matatu dakika ya 12, 19 na 35, pamoja na Guillermo Trujillano aliyetikisa nyavu dakika ya 25, 40 na 51.

Katika mechi hiyo Cruz ndiye aliibuka nyota wa mchezo huo baada ya kufikisha mabao matano.

Katika Kundi E, Uzbekistan nayo ilipata ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Jamaica, huku Sukhrob Sadirjanov akitawala mchezo kwa kufunga hat-trick. Jamaica ilianza kwa kasi na kupata mabao kupitia Kelvin D Brown dakika ya nane na 25, lakini Laziz Abduraimov aliisawazishia Uzbekistan dakika ya tisa kabla ya Sadirjanov kuanza kugeuza matokeo kwa bao dakika ya 30.

Sadirjanov aliendeleza ubora wake kipindi cha pili kwa kufunga dakika ya 47 na 58 na kukamilisha hat-trick yake, kabla ya Amirkhon Erkinov na Akhrorbek Ravshanbekov kuongeza mabao dakika ya 79 na 90+2.

Hat-trick nyingine ilipatikana Kundi F, ambako nahodha Jona Benkotic aliiongoza Croatia kuichapa Tajikistan mabao 4-0. Benkotic alifunga dakika ya sita, 50 na 56, kabla ya Jakov Dedic kuongeza bao la nne dakika ya 59. Katika mchezo mwingine wa kundi hilo,

Mechi nyingine zinazoendelea muda huu Italia dhidi ya Ivory Coast katika Kundi E, ambako Italia ipo mbele kwa bao 1-0 dakika ya 38, huku Mali ikitarajiwa kuvaana na Ubelgiji na Vietnam kukutana na New Zealand katika Kundi G.

Mechi zingine zinaendelea muda huu na tayari Senegal ipo mbele kwa mabao 9-0 dhidi ya Cuba dakika ya 79.