Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

“Chama na Dube wamegeuza dhihaka kuwa heshima”

CHAMA Pict


INGAWA mshambuliaji wa TRA United, Adam Adam amekaa nje kwa muda akiuguza jeraha la goti aliloumia mechi ya nusu fanali ya Kombe la Mapinduzi 2026 dhidi ya Yanga iliyochezwa Januari 6, 2026 huko Zanzibar, lakini hajamzuia kufuatilia kinachoendelea Ligi Kuu Bara.


Adam anayetarajia kujiunga na timu wiki hii, miongoni mwa vitu vinavyomvutia ni kiwango kinachoonyeshwa na kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama na straika wa Yanga, Prince Dube.


Akimzungumzia Chama kutoka kubezwa na mashabiki hadi kupewa heshima aliyokuwa nayo mwanzo, amesema kama isingekuwa uimara wa akili kukubali kujituma asingeweza kufikia hatua hiyo inayostahili kuigwa na kila mchezaji anapopitia changamoto.

CHAM 01

“Wakati Chama anaondoka Yanga kwenda kujiunga na Singida BS, ilionekana ndiyo mwisho wa thamani yake, hata wakati anarejea Simba hakuonekana ni mchezaji anayeweza akawa chachu katika timu, lakini kaamua kujituma na sasa anaimbwa kila kona, hilo ni funzo kufanya kile kisichowezekana kuwezekana,” amesema Adam na kuongeza:

“Kwa upande wa Dube goli limefunguka kwa upande wake na kiwango chake kipo juu, maana kuna kipindi alipitia cha kukosa mabao, jambo ambalo linaumiza zaidi hasa kwa nafasi ya ushambuliaji, lakini alijipa moyo akaamua kufanya bidii na sasa ni msaada kwa klabu ya Yanga.”

Dube anamiliki mabao tisa na asisti mbili katika Ligi Kuu Bara ambapo msimu uliopita alimaliza na mabao 13 na asisti nane, huku Chama akiwa na mabao matano na asisti tatu, huku 2024-2025 akiwa na Yanga alifunga mabao sita na asisti tatu, jambo ambalo kwa upande wa Adam anaona wana takwimu nzuri na bidii inaonekana kwao.

CHAM 02

Msimu wa 2023-2024, Adam alimaliza na mabao saba, jambo ambalo liliwavutia viongozi wa Azam kumsajili, hata hivyo wakamtoa kwa mkopo kwenda Tanzania Priosons, alipomaliza mkataba akaibukia TRA msimu huu ambao majeraha yalimtoa katika mstari wa ushindani.

“Mchezaji anapokuwa nje vitu vingi vinapungua kwani anahitaji muendelezo wa kucheza mara kwa mara, naendelea vizuri lakini siwezi kufanana na wale ambao walikuwa wanacheza kiufipi,” amesema.

Wachezaji ambao amewazungumzia Adam, wamekuwa na namba nzuri msimu huu kwenye ligi ambapo Dube amehusika kwenye mabao 11 akifunga tisa na asisti mbili, wakati Chama amehusika nayo kumi akifunga sita na asisti nne.