Yaliyoiangusha Simba Queens CECAFA
Muktasari:
- Timu hiyo imeaga mashindano baada ya kumaliza vibaya kampeni yao Kundi C la michuano hiyo inayoendelea, jijini Kigali, Rwanda.
HAIKUWA bahati kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kuaga mashindano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA kuwania tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu hiyo imeaga mashindano baada ya kumaliza vibaya kampeni yao Kundi C la michuano hiyo inayoendelea, jijini Kigali, Rwanda.
Simba ilianza kwa kuifunga Top Girls Academy ya Burundi mabao 2-0, mechi ya pili ikapoteza 2-1 dhidi ya Kenya Police Bullets, ambayo pia iliiondoa Wanamsimbazi hao mwaka 2024 nusu fainali ya mashindano hayo kwa mabao 3-2.
Miaka ya karibuni timu hiyo haijawa na kiwango bora katika mashindano hayo na tan-gu ilipofika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2022 haijashiriki tena michuano hiyo na mwaka 2024 ilifika nusu fainali ya Cecafa ikimaliza nafasi ya nne.
Mwanaspoti limekuchambulia baadhi ya sababu za timu hiyo kuondolewa kwenye mashindano hayo.
CHANGAMOTO SAFARI
Baada ya kuwepo Kenya kwa siku saba ikijiandaa na michuano hiyo, ilipanga kwenda Rwanda kwa usafiri wa basi, lakini likapata changamoto na hivyo kulazimika kuondoka kwa mafungu kwa ndege.
Timu hiyo ilifika siku moja kabla ya michuano hiyo iliyoanza Agosti 21 na hivyo kuto-kana na uchovu wa safari, inatajwa kama moja ya sababu za kufanya vibaya na baadhi ya wapinzani wao waliofika mapema, walipata nafasi ya kuzoea mazingira.
BUILD-UP HAIKUWA NZURI
Ilivyokuwa ikianzisha mashambulizi kutokea nyuma hawakuwa na njia za kupita eneo la kati kwenda kwa wapinzani na kujikuta wakitafuta njia nyingine kwenda mbele.
Dhidi ya Top Girls wapinzani hao walitumia vyema eneo la katikati wakizuia pasi am-bazo zingewaruhusu Simba kuingia eneo lao.
Simba ilikosa huduma nzuri ya Vivian Corazone ambaye alitoka kuwa majeruhi msimu uliopita na hata mechi ya tamasha la Simba Day hakutumika.
Kutokana na changamoto hiyo, hakuonyesha kiwango chake eneo hilo kwani alikosa utulivu wa kutoa pasi na kupeleka kwa washambuliaji, Aisha Mnunka na Mary Siyame ambao wangekuwa na kazi rahisi ya kupata mabao.
PEMBENI HAKUKUWA NA MADHARA
Simba ilijaribu kutumia mabeki na mawinga wa pembeni kupandisha mashambulizi (overlaps) lakini ilikosa mwendelezo na kushindwa kuwafanya Top Girls waanze kuvurugika, hivyo, mashambulizi yakawa na uelekeo mmoja.
Dhidi ya timu inayofunga nafasi, Simba ilipaswa kubadilisha upande wa mashambu-lizi kwa haraka, kuongeza kasi ya pasi na kuna wakati ilifanya hivyo lakini kwa kiwan-go kidogo.
Pia ilishindwa kujilinda baada ya kutoka kushambulia na walipopoteza mipira na baadhi ya wachezaji walichelewa kurudi kukaba wakati wanashambuliwa kwa kush-tukiza. Kwa kifupi walionekana hawako fiti.
Hapo ndipo Top Girls na Kenya Police zilipopata nafasi ya kushambulia kabla Simba haijarudi kwenye muundo wake.
Pia katika mechi dhidi ya Kenya Police iliingia kwa papara ya kushambulia zaidi na licha ya kutawala kwa asilimia kubwa (63) na kutengeneza nafasi kadhaa, ilishindwa kuzitumia kuwa mabao.
MAKOSA BINAFSI, UFANISI
Dhidi ya Kenya Police, moja ya makosa yaliyoigharimu ni la eneo la beki.
Matrtha Emedot wa Police alitumia makosa ya kipa wa Simba, Ruth Aturoa mbaye hakuwa na maelewano mazuri na beki wa kushoto Asha Omary na kuipa faida Police.
Tatizo lingine lilionekana kwenye uzoefu na baadhi ya nyota wa Simba wakiwamo Asha Omary na Aturo ambao ni mara ya kwanza kucheza katika michuano hiyo, sam-bamba na Hellen Kutdanize anayeidakia timu ya taifa ya Uganda.
Pia Simba ilikosa mtu wa kubadili matokeo na ni wazi kazi hiyo ingefanywa vyema na mshambuliaji kama Jentrix Shikangwa ambaye aliondoka kikosini hapo msimu uliopita akijiunga na FC Masar ya Ligi Kuu ya Wanawake Misri.
Mshambuliaji huyo alikuwa na mchango mkubwa Simba, pia alikuwa na uwezo wa kunusa hatari na kubadilisha mechi kwenye wakati ambao Simba ilikuwa inahitaji ma-tokeo.
INAJITAFUTA
Simba ilishiriki michuano hii mara ya mwisho mwaka 2024 na iliishia nusu fainali, hu-ku mafanikio makubwa ni kubeba taji hilo mwaka 2022 na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.
Hata hivyo, imekuwa ikisuasua katika michuano mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu ya Wanawake Bara na hivyo kushindwa kufuzu kwenye michuano hiyo na mwaka jana Tanzania iliwakilishwa na JKT Queens.
Simba inapaswa kujipanga haswa katika michuano hiyo endapo itafuzu msimu ujao, kwani imekuwa timu tishio ukanda huu na matarajio ya wengi ni kufika fainali na hata kubeba taji kutokana na uzoefu iliyyonao katika michuano hiyo, tofauti na wapinzani wao wa Tanzania ikiwamo Yanga Princess ambayo haijawahi kushiriki.
Simba pia imekutana na timu zenye uzoefu na michuano hiyo zikiwamo, CBE ya Ethi-opia ambayo imeshiriki mara ya tano, Kenya Police, Yei Joints ambao ni mara yao ya tano, Kenya Police mara nne.
MAKUNDI YA CECAFA
Michuano ya mwaka huu imehusisha timu 10 zilizogawanywa katika makundi matatu.
Kundi A limekuwa na timu nne, wakati Kundi B na C yakiwa na tatu kila moja.
Kundi A lilikuwa na wenyeji Rayon Sports ya Rwanda, Yei Joint Stars ya Sudan Kusi-ni, Mafunzo Queens ya Zanzibar na Denden FC ya Eritrea.
Katika kundi hilo, Yei Joint Stars imekuwa miongoni mwa timu zilizofanya vizuri, ikifuzu hatua ya nusu fainali baada ya kumaliza kileleni.
Rayon Sports na Yei Joint Stars zilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi yao ya mwisho, matokeo yaliyoiwezesha Yei kutangulia kufuzu hatua hiyo.
Kundi B lina CBE ya Ethiopia, Kawempe Muslim Ladies ya Uganda na FC Ujeco ya Djibouti.
CBE iliingia kwenye mashindano ikiwa miongoni mwa timu zenye uzoefu mkubwa baada ya kutwaa ubingwa wa CECAFA mwaka 2024, huku Kawempe Muslim Ladies ikiwa inashiriki kwa mara ya pili.
Kundi C, ambalo Simba Queens imeondolewa, lilikuwa na Simba Queens ya Tanza-nia, Kenya Police Bullets ya Kenya na Top Girls Academy ya Burundi.
Mfumo wa mashindano unaweka nafasi ya nusu fainali kwa vinara wa Kundi B na C pamoja na timu mbili bora kutoka Kundi A. Mshindi wa Kundi A anakutana na mshindi wa Kundi C, wakati mshindi wa Kundi B anakutana na mshindi wa pili bora wa Kundi A.
Bingwa wa CECAFA ndiye atakayepata tiketi ya kuiwakilisha ukanda huo katika Ligi ya Mabingwa Afrika ya Wanawake.