Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uungwana na ushabiki bora katika soka

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Ubingwa huo ulitangazwa baada ya kuifunga JKT mabao 3-0 Kwenye Uwanja wa Isamuyo jijini Dar es salaam na moja ya tukio kubwa lililosambaa mitandao ni ajali ya kimchezo aliyopata kiungo wa mabingwa hao mara tano mfululizo, Pacome Zouzoua katika kipindi cha pili ambayo imeacha majeraha makubwa katika mguu wake.

WAKATI tukiendelea na hekaheka za mashindano ya Kombe la Dunia 2026 yanayofanyika Canada, Marekani na Mexico katika hatua ya mtoano,  Tanzania jana Yanga ilitangazwa bingwa wa Ligi Kuu Bara 2026.

Ubingwa huo ulitangazwa baada ya kuifunga JKT mabao 3-0 Kwenye Uwanja wa Isamuyo jijini Dar es salaam na moja ya tukio kubwa lililosambaa mitandao ni ajali ya kimchezo aliyopata kiungo wa mabingwa hao mara tano mfululizo, Pacome Zouzoua katika kipindi cha pili ambayo imeacha majeraha makubwa katika mguu wake.

Tukio hilo lilishtua watu wengi ikiwamo mashabiki wa timu zote mbili ambao walionyesha uungwana wa kimchezo yaani fair play, kwa kumfariji staa huyo.

Ushabiki bora wa kuunga mkono mchezaji huyo kuletewa huduma haraka na madaktari wa timu waliokuwa na wepesi wa hali ya juu waliingia na kumpa huduma za awali za dharura.

DOKT 04

Soka ni mchezo mkubwa duniani ambao unaingiza mamilioni ya fedha huku ukibeba hisia kali za mashabiki ambao siku zote hutaka timu zao zishinde na kubeba ubingwa.

Pamoja na hayo yote, linapokuja suala la uhai wa mtu au afya ya mtu hapo ndipo uungwana na ushabiki bora unahitajika, vinginevyo mchezo huu ungekosa utu kwa majeruhi au wanaopata matatizo ya kiafya.

Mchezaji muungwana humjali mpinzani wake na pale anapopata tatizo la ajali ya kimchezo au apomfanyia faulu 'rafu'. Kufanya hivyo ndiyo kunaleta faraja na kumweka katika hisia nzuri majeruhiwa.

Ushabiki bora ni pale shabiki anapotambua kuwa pamoja na uwepo wa upinzani mkali wa mchezo lakini bado anawajibu wa kujali na kutoa msaada pale inapotokea mchezaji au yoyote yule anapoumia au kuumwa au kuwa na tishio la uhai.

DOKTA 01

Ndiyo maana hata katika kombe la dunia FIFA  2026 hivi sasa kuna mabango mengi yenye ujunbe wakusisitiza fair play katika mchezo wa soka.


Umuhimu wake ni huu hapa

Fair Play ni kitu kipana katika michezo ambacho kimebeba uthamani wa mambo mengi ambayo si tu kwa michezo bali hata mambo ya kimaisha ya kila siku.

Ushindani wenye uungwana katika michezo unabeba heshima, utu, urafiki, umoja, hamasa ya timu, heshima kwa kanuni na sheria za michezo zilizoandikwa na zile zisizoandikwa kama vile uaminifu, mshikamano, uvumilivu, kujali, ubora na furaha.

Hivyo hapa tunapata picha kuwa mambo mengi haya ndiyo yanajenga msingi mkuu wa fair play katika michezo hatimaye michezo inakuwa si uadui bali ni burudani.

Tafiti kadhaa zimawahi kuja na majibu kuwa uungwana wa kimchezo au maarufu zaidi kama Fair Play ni moja ya nyenzo muhimu ya kupunguza majeraha yasiyo ya lazima michezoni.

Moja ya tafiti hizo ni ile iliyofanyika 2018 ni ile iliyofanywa na taasisi ya Sport Medicine Psychology Laboratory ya Marekani ambayo ilijikita kutafiti fair play na upunguzaji kasi ya majeraha ya kimichezo kwa wanamichezo vijana kwa kuhamasisha tabia za kiungwana.

DOKT 03

Nyenzo ya Fair Play ndiyo inamfanya mchezaji wa upinzani kuutoa mpira nje au kusimamisha mpira ili mpinzani au mwenzake apate huduma ya kwanza.

Mfano mzuri wa uungwana mchezoni umewahi kuonyeshwa katika soka kwa vitendo Desemba 2000 na mchezaji wa west Ham, Paolo Di Canio dhidi ya Everton katika mechi ya ligi kuu EPL.

Katika mechi hiyo, kipa wa Everton, Paul Gerrard alipiga mbizi ili kupokonya mpira lakini aliumia wakati alipokuwa akifanya hivyo hatimaye mchezaji wa West Ham aliunasa na kutoa pasi.

Di Canio ambaye alikuwa katika nafasi nzuri alipokea pasi hiyo akiwa yeye na lango likiwa wazi kwani kipa alikuwa hayuko eneo hilo akigaragara kwa maumivu ya jeraha.

Wengi walitarajia angelifunga lakini hakufanya hivyo, badala yake aliutoa mpira nje ili kutoa nafasi kwa watoa huduma ya kwanza waje uwanjani ili kumpa kipa huyo huduma.

Tukio hili lilikuwa ni moja ya matukio ya juu ya kiungwana katika soka na liliishia kwa Di Canio kupata tuzo ya FIFA Fair Play Award mwaka uliofuata 2001.

Vile vile, hata inapotokea mchezaji hakuweza kurudi uwanjani basi huweza kupata faraja kutokana na vitendo vya kiungwana ambavyo huonyeshwa na mpinzani wake na wachezaji wenzake.

Ukiacha uungwana, ushabiki bora nao una mchango wake kwani kitendo cha mashabiki kuonyesha kumjali na kumuunga mkono mchezaji aliyejeruhiwa humpa faraja na kumpa tiba ya kiakili.

Endapo ingelikuwa mashabiki wanamzomea na kumpa maneno makali mchezaji majeruhi ina maana ingeliweza kuwapa mpasuko wa kihisia hatimaye mtikisiko wa kiakili ikiwamo kupata msongo wa mawazo.

Mchezaji majeruhi anapokuwa amejeruhiwa na huku anapata matatizo ya kiakili kama msongo wa mawazo ina maana kuwa anakuwa amebeba jeraha la kimwili na kiakili.

Vitu hivi vikiwepo mwilini tayari inakuwa mwili hauna afya njema na matokeo yake anaweza kuchangia mwili kuwa dhaifu na kutokupona kwa wakati.

Tukio la kuzimia kwa Christian Eriksen na kupewa faraja na uungwaji mkono  na mashabiki wakati anapatiwa huduma ni ishara hata mashabiki wenye hisia kali wanatambua uhai wa mtu ni zaidi ya vyote.

Tumeshudia mashabiki mbalimbali duniani wakitumia muda mwingi katika kuta za mitandao ya kijamii kuwapa maneno ya faraja wachezaji waliopata majeraha mabaya na kutolewa uwanjani.

Mamia ya wachezaji, mashabiki, makocha na wadau wa soka Tanzania waliungana pamoja kumpa faraja Pacome kwa kumwandikia maneno mazuri ya kumfariji katika kuta za mtandao wake wa kijamii.

Na vitendo hivi vinafanywa si tu kwa mashabiki wa mchezaji huyo bali pia na wale ambao ni wapinzani wao, hii inaonyesha mshikamano wa kiungwana wa mashabiki kwa wachezaji wanaopata majeraha.

Uungwana wa kimichezo yaani fair Play na ushabiki bora vitabaki kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya michezo kuliko timu kushinda au kuchukua ubingwa.

Katika tukio hilo la ajali mbaya ya kimchezo wachezaji wa timu zote mbili walionyesha mshikamano wa hali ya juu kwa kumfariji mchezaji huyo.

DOKT 02

Chukua hii

Majeraha aliyopata Pacome huenda yakamweka nje kwa muda mrefu, moja ya mbinu muhimu ya kuweza kumsaidia kupona kwa wakati ni kupata matibabu sahihi kutoka kwa wataalam wabobezi wa majeraha ya michezo.

Ungwana katika soka ni muhimu sana katika kusaidia kuwaepusha wanasoka na majeraha mabaya yatokanayo na mchezo. Spoti Dokta inatakiwa Pacome uponaji wa haraka.