Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unamuonaje Schwarzenegger? Chukua hii

ANORD Pict

Muktasari:

  • Kama unavyowasikia watoto wa sasa wakiitana majina ya Ronaldo au Messi wanapocheza chandimu mitaani, ndivyo ilivyokuwa kwa kizazi cha zamani ambapo jina la Schwarzenegger miaka ya 1970 hadi 2000 lilitawala.

LOS ANGELES, MAREKANI: UNAMKUMBUKA mkali wa filamu za mapigano Arnold Schwarzenegger? Mwamba alicheza picha kibao ambazo zilimfanya kuwa bilionea, na kumfanya azungumzwe sana katika mitaa na vijiwe vingi vya Bongo enzi zake akianzia katika mashindano ya kujenga mwili (bodybuilder).

Kama unavyowasikia watoto wa sasa wakiitana majina ya Ronaldo au Messi wanapocheza chandimu mitaani, ndivyo ilivyokuwa kwa kizazi cha zamani ambapo jina la Schwarzenegger miaka ya 1970 hadi 2000 lilitawala.

Kama humkumbuki au unataka kumfuatilia ili umjue cheki filamu zake za mapigano za Terminator (1984), Terminator 2: Judgment Day (1991) na Predator (1987) utayaona mavitu yake. Kwa sasa Schwarzenegger ana umri wa miaka 78 akiwa anaonekana kuzeeka, lakini mwili wake ungali mkakamavu kutokana na kuendelea kuishi akifanya mazoezi ya nguvu.

Nyota huyo aliyezaliwa Julai 30, 1947 amezungumzia siri ukakamavu wake wakati akitarajia kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kesho, kuadhimisha umri wa miaka 79, na hiki ncho alichosema.

ANO 04

KANUNI YA TIZI

“Hii ndiyo kanuni ninayoifuata ili nijisikie kijana nikiwa na miaka 78. Nilipokuwa nikishindana kujenga mwili (bodybuilder), nguvu zilikuwa na maana moja tu; uzito zaidi. Mazoezi makali zaidi. Maumivu zaidi. Falsafa hiyo ilinisaidia kushinda mataji 13 ya dunia.

Lakini, kadiri muda ulivyopita, niliongeza jambo jingine katika falsafa hiyo ambayo ni nidhamu ya kuupa mwili muda wa kupona, kuendana na mabadiliko na kuendelea kusonga mbele hata pale ambapo kusonga mbele kunakuwa kugumu zaidi.

“Kwa uzoefu wangu, hicho ndicho kinachowafanya mamilioni ya watu washindwe kuishi maisha yao kikamilifu, kwa sababu maumivu huwafanya wakate tamaa kabla hawajajifunza mwili wao bado unaweza kufanya nini. Nilipotimiza miaka 70, watu walianza kuniuliza kwa nini bado nilikuwa nafanya mazoezi. Sasa ninapokaribia kutimiza miaka 79, maswali hayo yameongezeka zaidi wakiuliza “kwa nini bado unaenda mazoezini? Je, haujaona ni wakati wa kupumzika?”

ANO 05

“Watu wengi hudhani kuwa mazoezi ya mwili yana mwisho. Hayana. Siyo kila siku mazoezi huwa mazuri. Kuna siku kufika tu kwenye eneo la mazoezi ndiyo ushindi wenyewe. Huo unanitosha. Kadiri tunavyozeeka, mara nyingi tunasimulia hadithi hii, maumivu hayaepukiki, mwili kukakamaa ni jambo la kawaida na maisha madogo ya polepole ndiyo gharama ya kuzeeka.

“Nimesikia simulizi hiyo kutoka kwa watu wanaozunguka maisha yangu. Nimefanyiwa upasuaji wa mabega, upasuaji wa moyo na kubadilishiwa nyonga. Ninafahamu vizuri namna ilivyo kuambiwa kwamba mwili wako siyo kama ulivyokuwa zamani. Kwa kifupi, kuzeeka siyo jambo la kufurahisha.

“Lakini sijawahi kukubali kwamba kuzeeka kunamaanisha kuishi maisha mafupi na ya polepole. Baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo, madaktari waliniambia kwamba kunyanyua vyuma vizito haikuwa tena chaguo salama. Kwa mtu aliyejenga maisha yake kwa kusukuma mipaka ya uwezo wake, huo ulikuwa ukweli mgumu kuukubali. Nilirudi ukumbini kufanya mazoezi na ilinibidi nijifunze upya kila kitu.

ANO 02

“Mara ya kwanza niliponyanyua vyuma tena, nililazimika kutumia uzito mdogo kuliko nilivyozoea. Harakati ambazo nilikuwa nimezifanya kwa miongo kadhaa ghafla zilihitaji umakini zaidi na uvumilivu mkubwa zaidi. Lakini, zaidi ya yote, hali hiyo ilinifanya nitambue jinsi ilivyo rahisi kuruhusu vikwazo vikatawale maisha yako ikiwa hutapambana navyo kwa makusudi.

“Ni kweli, kuna asubuhi ambazo sitaki hata kuamka kitandani. Viungo vyangu huhisi vizito na mazoezi huonekana kuwa jambo la mbali. Katika asubuhi kama hizo, sisubiri motisha. Naamka tu. Na wakati fulani nikiwa safarini kwenye baiskeli au baada ya kufanya seti chache za mazoezi, narudi katika hali yangu.

“Nimeanza kuona mtindo huu kwa watu wengi wanaonizunguka. Siku moja wanaacha kutumia ngazi kwa sababu magoti yanauma. Wanaghairi matembezi ya jioni baada ya chakula kwa sababu wanahisi mwili umekakamaa. Wanaanza kuepuka mambo ambayo zamani yalikuwa rahisi.

ANO 01

Polepole, bila wao kutambua, dunia yao inaanza kuwa ndogo na mipaka yao inaanza kujitokeza.

“Ninaliona hili wazi katika maisha yangu mwenyewe. Ninaendelea kuwafundisha watu wa rika zote katika safari zao za mazoezi kupitia programu yangu ya Pump Club. Ninacheza na wajukuu zangu ambao ni kipimo halisi kabisa cha uwezo wangu wa kusogea. Muda mrefu uliopita, mazoezi yaliacha kuruhusu umbo langu lionekane bora. Sasa nafanya mazoezi ili niweze kuendelea kufanya mambo yenye umuhimu kwangu.

“Maumivu na mwili kukakamaa vinapoamua kama unaweza kusimama kutoka kwenye kiti, kupanda ngazi au kwenda sambamba na familia yako, hapo uhuru wako wa kujitegemea unakuwa hatarini. Utafiti uko upande wangu, kufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kupunguza maumivu, kuboresha uwezo wa mwili kufanya kazi, kujenga nguvu, kuboresha na kulinda ubora wa maisha.

ANO 06

“Nimekuwa nikifanya mazoezi kwa zaidi ya miongo sita, na mazoezi ninayofanya leo ni tofauti kabisa na yale niliyokuwa nikifanya nikiwa na umri wa miaka 20. Natumia vyuma vyepesi zaidi, lakini narudia mara nyingi zaidi, huku nikipunguza muda wa kupumzika kati ya seti ili kudumisha ukali wa mazoezi.

“Ninaendesha baiskeli badala ya kukimbia ufukweni. Ninapoenda kuteleza kwenye theluji, ninaishia katikati ya siku. Sichanganyi tena nidhamu na ukaidi. Sasa utaratibu wangu wa mazoezi unalenga udhibiti, mwendelezo na kuhakikisha kwamba bado ninaweza kuendelea kuisongelea kesho.

Njia yangu imebadilika, lakini dhamira yangu imebaki ileile.

ANO 07

“Kwa miaka mingi nimetumia kauli ya shujaa wangu Teddy Roosevelt (rais wa 26 wa Marekani) aliyesema “ukipumzika, utapata kutu.” Watu hucheka kwa sababu kauli hiyo ni ya moja kwa moja. Lakini, kadiri ninavyozeeka, ndivyo ninavyoona ukweli wake. Huhitaji kujisalimisha kwa dhana za zamani kwamba umeshapita hatua ya kuweza kubadilika.

ANO 03

“Nimekutana na watu wenye umri wa miaka ya 60 na 70 katika Pump Club ambao walibadilika kutoka kushindwa hata kufanya jaribio dogo la mazoezi kwa ajili ya miili yao hadi kushiriki mashindano ya kuinua vyuma. Utafiti unaonyesha kuwa hata watu wenye umri wa miaka ya 80 na 90 bado wanaweza kuongeza nguvu zao.

“Tunahitaji mazungumzo ya wazi zaidi kuhusu kuzeeka na kuishi maisha marefu. Kusonga siyo anasa ya vijana au wale wasiokuwa na maumivu.


Kusonga ni sehemu ya kutunza maisha. Ndiyo njia tunayolinda uhuru wa kujitegemea, ustahimilivu na uwezo wa kuendelea kufanya mambo tunayoyapenda. Hivyo ndivyo kurudi kuwa unavyopaswa kuonekana.”