Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukipanda ndege ya supastaa Ronaldo utagoma kushuka!

Ronaldo Pict

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa Ureno, mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa, mwaka jana aliongeza kwenye vyombo vya usafiri, aliponunua ndege aina ya Bombardier Global Express 6500.

LONDON, ENGLAND: UNAPOKUWA supastaa kama Cristiano Ronaldo, unahitaji usafiri wa maana kama wa ndege binafsi ili kwenda sambamba na staili yako ya maisha.

Gwiji huyo wa Ureno, mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa, mwaka jana aliongeza kwenye vyombo vya usafiri, aliponunua ndege aina ya Bombardier Global Express 6500.

Hakika ndege hiyo imemgharimu Ronaldo pesa nyingi, Pauni 61 milioni huku ikirembwa na kunakshiwa na vitu mbalimbali vinavyomtambulisha mwanasoka huyo aliyewahi kuzichezea Sporting CP, Manchester United, Real Madrid, Juventus na sasa Al Nassr.

RO 02

Hivi karibuni ndege hiyo iliyonekana Uwanja wa Ndege wa Manchester na kuzua uvumi wa kuhusu usajili. Hata hivyo, haikufahamika kwa nini ndege hiyo ilitua kwenye jiji hilo la Manchester, maskani ya timu yake ya zamani ya Man United. Na kilichogundulika baadaye ni kuna dirisha la ndege hiyo kioo chake kilionekana na ufa, hivyo wanahitajika mainjia wa ndege kurekebisha tatizo hilo kabla ya kuanza safari.

Jambo hilo litakuwa pigo kwa Ronaldo na mpenzi wake, mrembo Georgina Rodriguez, ambao wamekuwa wakipenda sana kutumia usafiri huo wa anga kwa ndege yao binafsi kwenye mambo yao.

Lakini, ushawahi kujiuliza kwa nini Ronaldo na mrembo wake huyo, Georgina wanapendelea zaidi usafiri wa ndege yao hiyo, ndani kuna nini? Yaliyomo ndani ya ndege ya Ronaldo.

RO 01

Ndege ya kipekee kabisa

Kitu cha kwanza kabisa kinachotofautisha ndege binafsi ya Ronaldo na za mastaa wengine, hii unaweza kusafiri kwa safari za mbali. Ndege hiyo ina uwezo wa kusafiri zaidi ya saa 18 bila ya kuhitaji kutua.

Ina uwezo wa kupaa kwa umbali wa maili 6,600, hiyo ina manaa unaweza kupaa kutoka Hong Kong hadi London bila ya kusimama kuhitaji kuongeza mafuta. Hivyo kwa ishu ya kutoka Riyadh hadi kwenye Jiji la Manchester, huo ulikuwa umbali wa maili 2,800. Injini ya ndege hiyo ni Rolls-Royce, inakimbia kwa spidi ya Mach 0.90. Hata mabawa ya ndege hiyo yametengenezwa kuhimili hali yoyote ile ya hewa.

RO 03

Ukipanda ni starehe tu

Ndege hiyo ya Ronaldo ina mambo mengi ya starehe ambayo yanawafanya abiria wake kufurahia safari.

Kuanzia ngazi zake zimetengenezwa kisasa sana, huku kuna majiko ya kifahari na ndani kuna oven, microwave na hata mashine ya kutengeneza kahawa. Kuna mabafu yenye vioo vikubwa, majacuzi na mambo mengi matamu, ambayo yanafanya abiria wasiwe na uchovu wakiwa angani wakati wa safari.

Ronaldo na mrembo Georgina hawatakuwa na shida ya nguo zao zinawekwa wapi ndani ya ndege hiyo, kutokana na kuwapo kwa makabati maalumu, ambayo pia wanatumia kuweka vito vya thamani.

Ukiweka kando vyumba vya kifahari vya Ronaldo na mpenzi wake, kuna vyumba vya wafanyakazi wa ndege hiyo pamoja na ukumbi wa mikutano na kuna meza ambazo zinakunjika pamoja na chumba cha kubadili mavazi. Ndege hiyo ya Ronaldo inajitosheleza, ina kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya safari za kustarehe.

RO 04

Mambo ya kuburudika

Kwa safari za umbali mrefu kwenye ndege, mambo ya burudani ni muhimu sasa na bahati nzuri kwa Ronaldo na familia yake ndege yake ya Global Express 6500 imeheshimu mambo yote hayo.

Kwanza, kuna televisheni kubwa kabisa 4K UKHD TV, ambayo utatazama filamu unazopenda wakati ukiwa safarini. Ndani ya ndege hiyo kuna intaneti yenye kasi zaidi na unaweza kusikiliza muziki wa kwenye mitandao bila ya wasiwasi wowote ukiwa safarini. Kama ukiwa na vifaa vyako vya umeme kama simu na kompyuta mpakato wala hauna shida zitaisha chaji, kuna poti kibao za kuchaji. Kwa kifupi unaposafiri kwenye ndege ya Ronaldo hakuna muda utakuwa umechoshwa na safari.