Manqoba angepunguza spidi kidogo
Muktasari:
- Ndicho kijiwe hapa kinaamini ndiyo kimemtokea jamaa yetu Malume ambaye sasa hivi ameonyeshwa mlango wa kutokea pale Jan
SPIDI ya Manqoba Mngqithi ilikuwa kubwa sana bhana baada ya kuja Bongo. Alitakiwa apunguze kidogo. Unapoenda kuanza kazi mahali hautakiwi kuwa na mbwembwe zilizopitiliza maana baadaye zinaweza kutumika hizo hizo kukuhukumu.
Ndicho kijiwe hapa kinaamini ndiyo kimemtokea jamaa yetu Malume ambaye sasa hivi ameonyeshwa mlango wa kutokea pale Jan
Alipotua tu baada ya kuona watu wanapata tabu kulitamka jina lake, akawaambia kama vipi wanaweza kumuita kwa jina la utani la Mtekaji au Mporaji akimaanisha yeye ni jemedari hasa.
Kabla hata hilo jina halijakaa vizuri vichwani akaibuka na ile staili yake ya kuvichambua nje ndani vikosi na wachezaji wa timu pinzani kabla hawajakutana na timu yake.
Na vile alivyoanza kwa kugawa dozi tena akianzia katika mechi ya ngao dhidi ya Simba na kisha akaendelea katika ligi basi inawezekana alijiona ameshajihakikishia ulaji wake kwa wananchi ukizingatia walivyokuwa wakimuimba.
Lakini kumbe mikwara yote ile aliyokuwa akipiga na hata kufikia kuomba ubalozi wa bidhaa za bosi haikuwa kinga kwake ya kumwezesha kudumu Yanga kwa muda mrefu.
Ilipaswa zile mbwembwe zake ziende sambamba na mpira mkubwa na matokeo mazuri ambayo timu inayapata bila kushikilia roho muda wote.
Lakini unawapiga watu samjo halafu watu wanatoka uwanjani baada ya dakika 90 wakiwa hawana furaha hata kama wameshinda, Manqoba asingeweza kutoboa.