Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SUPERCLASICO; Dabi isiyo ya Messi, lakini ya Maradona

SUPER Pict

Muktasari:

  • Na tangu gazeti la Observer Sport Monthly la Uingereza lilipochapisha orodha ya mambo 50 ya michezo unayopaswa kufanya au kushuhudia kabla ya kufa, likiweka kutazama Boca Juniors ikicheza na River Plate mjini Buenos Aires katika nafasi ya kwanza mwaka 2004, dabi hiyo kubwa zaidi nchini Argentina imekuwa sehemu muhimu ya taswira ya soka duniani.

BUENOS AIRES, ARGENTINA: LA BOMBENERA inayojulikana kama Estadio Alberto J. Armando ni uwanja maarufu wa mpira wa miguu uliopo katika mtaa wa La Boca, jijini Buenos Aires, Argentina, na ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya soka ya Boca Juniors.

Hilo ni dimba lililozinduliwa Mei 25, 1940 na lina uwezo wa kuchukua mashabiki kati ya 49,000 hadi 57,000, likiwa na muundo wa kipekee wa umbo la “D” wenye majukwaa yanayotoa sauti na msisimko wa pekee.

Asili ya jina “La Bombonera” inamaanisha “sanduku la chokleti”, jina ambalo ulipewa na mbunifu wake Viktor Sulcic baada ya kulinganisha muundo wa uwanja huo na sanduku la chokleti alilopewa zawadi. Uwanja huo unajulikana kwa mechi kali ya Dabi ya Superclásico dhidi ya River Plate, ambayo inahesabiwa kuwa mojawapo ya mechi kubwa na ya kusisimua wa kimichezo duniani.

Na tangu gazeti la Observer Sport Monthly la Uingereza lilipochapisha orodha ya mambo 50 ya michezo unayopaswa kufanya au kushuhudia kabla ya kufa, likiweka kutazama Boca Juniors ikicheza na River Plate mjini Buenos Aires katika nafasi ya kwanza mwaka 2004, dabi hiyo kubwa zaidi nchini Argentina imekuwa sehemu muhimu ya taswira ya soka duniani.

SUPE 06

Sifa zake za rangi, hamasa na hisia za kipekee zimeipa mvuto wa aina yake na wa kifahari zaidi, ikiambatana na mdundo na kishindo cha nyimbo za mashabiki zinazoimbwa kwa pamoja, karatasi za rangi zinazong’ara katikati ya moshi wa fataki zikifanana na rangi za jezi za timu, sakafu ya zege ikitikisika huku makumi ya maelfu ya mashabiki wakiruka kwa pamoja, polisi waliopanda farasi wakizunguka uwanja, vizuizi vya mashabiki vikichomwa moto, mafataki yakielekezwa kwa wachezaji; hakika ni hisia kufuatilia tukio hilo ukiwa jirani au katika eneo husika.

Mechi ya mwisho kati ya Boca Juniors na River Plate ilifanyika Novemba Mosi, 2026, ambapo Boca Juniors ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya mpinzani wake huyo.

Diego Maradona, gwiji wa zamani wa soka duniani, alikuwa shabiki mkubwa na nyota wa zamani wa Boca Juniors. Kwa Maradona aliyewahi pia kuifundisha timu hiyo kwa muda enzi za uhai wake hakusikia lolote inapotajwa Boca masikioni mwaka. Hata hivyo Lionel Messi, siyo shabiki wa Boca Juniors wala River Plate, bali ni shabiki wa Newell’s Old Boys. Upinzani kati ya Boca Juniors na River Plate unaojulikana kama Superclasico ni mkubwa sana nchini Argentina, lakini magwiji hao wawili wana historia tofauti linapokuja suala la klabu za nyumbani.

SUPE 05

Messi ni shabiki wa maisha wa Newell’s Old Boys kutoka mji aliozaliwa wa Rosario na alianza kucheza katika akademi ya vijana ya klabu hiyo akiwa na umri wa miaka sita au saba kabla ya kuhamia Barcelona, Hispania. Kuhusu Boca na River Plate, Messi amewahi kukana waziwazi kuwa na mapenzi au uhusiano wa kishabiki na timu hizo, ingawa utotoni aliwahi kufanya majaribio machache River Plate akiwa mtoto na kuwafunga wote katika mechi za kimataifa akiwa na Barcelona.

Kwa upande wa Maradona alikuwa shabiki sugu wa Boca Juniors. Ingawa alianza soka lake la kulipwa katika Klabu ya Argentinos Juniors, alikataa ofa nono ya mshahara kutoka River Plate 1981 ili ajiunge na Boca Juniors ambayo aliichezea kwa vipindi viwili (1981–1982 na 1995–1997), na alistaafu soka akiwa na jezi ya klabu hiyo. Alikuwa na chumba chake maalumu (private box) katika Uwanja wa La Bombonera ambako alikuwa akishangilia mechi zao kwa hamasa kubwa hadi mwisho wa maisha yake. Inasisimua, sivyo?

SUPE 04

SUPERCLASICO

Achana na Maradona na Messi na mapenzi yao kwa timu za nyumbani, Argentina, ambako Boca Juniors na River Plate ndizo zenye asilimia 70 ya wapenzi wa soka nchini humo, Superclasico ndiyo habari ya mjini kama ilivyo Dabi ya Kariakoo ya Simba na Yanga, Dabi ya Soweto kati ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates au ile ya Mashemeji ya Gor Mahia FC (K’Ogalo) na AFC Leopards (Ingwe).

Hata hivyo, mambo yamebadilika, na mchezo wa Novemba 1, mwaka huu, katika La Bombonera (uwanja wa Boca unaojulikana kama Chocolate Box), ulikuwa na mandhari tofauti kabisa. Tangu 2013, mechi za soka nchini Argentina zimekuwa zikichezwa bila mashabiki wa timu ngeni, hivyo kwa kuanzia, rangi za mashabiki zimepungua sana.

Kutokuwepo kwa kundi la mashabiki wa wapinzani kumekaribishwa na wengi, kukifanya kwenda kutazama mechi kuwa jambo linalofaa zaidi kwa familia na kuongeza upatikanaji wa tiketi kwa wanachama wa klabu.

Dabi ya kwanza ya Superclasico bila mashabiki wa ugenini iliyochezwa Uwanja wa Monumental 2013 unaotumiwa na River Plate ilishuhudia. Boca ikifunga bao kupitia Emmanuel Gigliotti na kuipa timu ya ugenini uongozi. Baada ya bao hilo ilisikika sauti katika eneo la waandishi wa habari mtu akianza kutamka herufi “G”, akiwa tayari kupiga kelele za furaha kushangilia bao, lakini ghafla akatambua kwamba “furaha ya wasiokuwa wenyeji ilipaswa kukandamizwa”.

Kwa miaka mingi, kutokuwepo kwa mashabiki timu ngeni kumeenda sambamba na kutokuwepo kwa waandishi wa habari wa ugenini. Sasa waandishi wa habari huketi kwenye meza zao katika usawa unaolingana na sehemu ya katikati ya jukwaa la mashabiki wa nyumbani, ambako moyo wa kundi kubwa la mashabiki waliopangwa na kuratibiwa, wanaojulikana kama La Doce, huongoza sehemu ya midundo na hisia za shangwe. Waandishi wa habari wakiwa wamevaa jezi za Boca hutukana na kushangilia pamoja na umati.

Katika mchezo wa majuzi, mvua ilitabiriwa kunyesha, hivyo Boca ilisambaza miavuli ya bluu na njano iliyofunguliwa kwa wakati mmoja na mashabiki kulingana na rangi ya moshi wa fataki uliofushwa na klabu hiyo. Awali, fataki hizo zilikuwa zikisafirishwa kwa siri na La Doce, ambao pia waliratibu kuachiliwa kwa maputo ya bluu na dhahabu wakati hasa wachezaji walipotoka kwenye handaki (mlango) la kuingilia uwanja. Jose Barritta alikuwa kiongozi maarufu wa La Doce miongo kadhaa iliyopita, na mwaka 1994 aliwahi kusimulia akielezea kwa kina kuhusu Superclasico kutokana na majukwaa yaliyogawanywa katika mara tatu na la katikati ndilo kitovu cha shughuli, akisema enzi hizo siku ya mechi ilikuwa balaa ambayo ingeishia kuwa janga, huku mashabiki wakipigana au kupigwa risasi na kuuawa baada ya mchezo.

Anasema, ilikuwa jambo la kawaida pia watu kuchukizana kutokana na matokeo na muda mfupi baadaye maandishi ukutani yangeonekana karibu na eneo yalipokuwa yakitokea machafuko jirani na uwanja yakiwa yameandikwa “River 2 Boca 2”, yakilinganisha maisha ya watu wawili na mabao mawili ambayo River ama ilikuwa imeifunga Boca na kupata ushindi au imepoteza kwa idadi hiyo ya mabao au zaidi ya hayo.


SUPE 01

DABI MBAYA

Nyakati hizo mara nyingi zilikuwa na msisimko au vifo ambavyo vilitokana na ushabiki na mapenzi ya watu kwa timu zao hizo mbili. Vifo katika Superclasico havikuwa jambo jipya hata wakati huo. Mwaka 1968, mashabiki 71, wengi wao wakiwa wa Boca walikandamizwa hadi kufa wakati lango moja la kutoka kwa mashabiki wa ugenini liliposhindwa kufunguka kikamilifu.

Tukio hilo lililojulikana kama Puerta 12, mengi ya yaliyotokea kwa hakika bado hayajulikani. Hata hivyo, El Grafico iliripoti kwamba mchezo wa mwaka uliofuata uliwashuhudia mashabiki wa Boca na River wakiimba kwa pamoja wakiwadhihaki polisi.

Katika siku hizo, makundi yote mawili yalikuwa na urafiki. Kiongozi wa kundi la Boca wakati huo, Quique, aliyekuwa akiendesha kibanda cha kuchoma nyama mkabala na uwanja, alinunua nyama kutoka kwa kiongozi wa kundi la River, “El Tano Mingo”, ambaye alikuwa mchinjaji.

Mara nyingi waliungana na kupambana dhidi ya makundi ya klabu nyingine hadi katikati ya miaka ya 1970, wakati uongozi ulipobadilika. Barritta alichukua uongozi wa La Doce 1981, wakati ambao ufa kati ya makundi hayo ulikuwa tayari mkubwa.


SUPE 03

MIAKA YA KARIBUNI

Mwaka 2018, Boca na River zilikutana katika fainali ya Libertadores, mashindano ya mabingwa wa soka ya klabu ya Amerika Kusini, ambapo rais wa Argentina, Mauricio Macri, alifikiri ingekuwa jambo la kufurahisha kuonyesha dunia jinsi Superclasico inavyoweza kuwa tamasha la rangi, hivyo mashabiki wa ugenini waliruhusiwa kurudi uwanjani katika mechi moja.

Baada ya basi la Boca kushambuliwa kwa mawe na udhibiti wa umati kuvurugika katika eneo la ndani linalozunguka Uwanja wa River, mashabiki walipewa maagizo makali ya kubaki mahali walipo kwa karibu saa tano huku mamlaka za serikali zikijadili hatua za kuchukua. Mechi ilifutwa na kwa namna ya kushangaza ikahamishiwa Madrid, ambako mtu anaweza kusema roho ya Superclasico imeendelea kubaki.

Na mchezo wa majuzi haukuwa wa kiwango cha fainali ya Libertadores. Mfumo wa sasa wa soka nchini Argentina una maana kwamba mchezo huo haukuwa na umuhimu mkubwa kwa kombe wala ligi, ingawa umeashiria kwamba ushindi wa Boca wa mabao 1-0 dhidi ya River, iliyokuwa imebaki na wachezaji tisa mwishoni, umeifanya Boca kupata nafasi katika mashindano ya Libertadores ya mwakani.


SUPE 02

CHIMBUKO LA UPINZANI

Klabu hizo mbili zilianzishwa mwanzoni mwa karne ya 20 katika kitongoji cha wafanyakazi cha La Boca jijini Buenos Aires, ambapo River Plate ilianzishwa 1901 na Boca Juniors 1905.

Inaelezwa kwamba mgawanyiko wa kitabaka mwaka 1925, River Plate ilihamia Kaskazini mwa jiji katika eneo la matajiri la Nunez na kubatizwa jina la Los Millonarios (mamilionea), huku Boca Juniors ikibaki La Boca na kuendelea kuwa klabu ya watu wa tabaka la wafanyakazi (Xeneizes), jambo lililochochea upinzani mkubwa ndani na nje ya uwanja.

Viwanja maarufu vya timu hizo ni Boca wanaotumia Uwanja wa La Bombonera unaojulikana kwa kelele na vurugu za mashabiki, huku River Plate wakichezea Estadio Monumental, uwanja mkubwa zaidi Amerika Kusini na wenye historia ya ukarimu, lakini wanapokuwepo wapinzani hao wawili lolote linaweza kutokea kwa wachezaji na mashabiki.

Katika historia tangu timu hizo zilipokutana mara ya kwanza 1913 zimecheza mechi rasmi 268, Boca Juniors ikishinda 95 na River Plate 88 ilhali sare ikiwa 88. Ushindi mkubwa kwa Boca Juniors ni ule wa Desemba 23, 1928 wa mabao 6-0 ilhali ule wa River Plate ulitokea Oktoba 19, 1941  mabao 5-1.