Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPUTANZA imeshindwa kufanya kazi yake na wala hakuna anayejali

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Marekebisho hayo yaliruhusu timu kufanya mabadiliko maalumu kwa mchezaji aliyejigonga kichwani (concussion) na akashindwa kuendelea na mchezo, hata kama timu ilishamaliza idadi ya wachezaji. Mathalani, kila timu inaruhusiwa kufanya mabadiliko hadi wachezaji watano.

KWENYE Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), liliifanyia marekebisho madogo sheria namba 3 ya mpira wa miguu katika zile 17 inayohusu mabadiliko ya wachezaji wakati wa mchezo.

Marekebisho hayo yaliruhusu timu kufanya mabadiliko maalumu kwa mchezaji aliyejigonga kichwani (concussion) na akashindwa kuendelea na mchezo, hata kama timu ilishamaliza idadi ya wachezaji. Mathalani, kila timu inaruhusiwa kufanya mabadiliko hadi wachezaji watano.

Sasa kama imeshamaliza wote watano halafu mchezaji mwingine akaumia kwa kujigonga kichwani timu hiyo itaruhusiwa kufanya mabadiliko mengine ya dharura.

Sheria hiyo ilianza kuwa rasmi tangu Julai Mosi, 2024 na kuanzia hapo mashikisho kadhaa duniani yanaitumia, kasoro Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na lile la Soka Tanzania (TFF). Hapa ndipo Chama cha Wanasoka Tanzania (Sputanza), kinapoingia. Chama hicho kilianzishwa maalumu kwa ajili ya kutetea maslahi ya wachezaji. Suala hili ni mojawapo.

PUM 01

Sputanza inapaswa kusimama imara na kupigania sheria hiyo kuanza kutumika nchini kwa faida ya afya za wachezaji. Wenzao, Chama cha Wanasoka wa Kulipwa England (PFA), ambako nchini kwao sheria hii inatumika wako kwenye vita ya mbele zaidi kuhusu sheria hii. Walipigana kwanza ije - ikaja na baada ya kuja sasa wanapigana vita mpya ya kesho. Wanataka badala ya mchezaji aliyeumia kwa kugongana kichwani afanyiwe mabadiliko ya muda. Yaani atoke, aingie mwingine kwa muda.

PUM 05

Halafu yule afanyiwe vipimo vya kiafya kama hajapata madhara makubwa basi arudi uwanjani na yule aliyeingia badala yake atoke. Unaweza ukaona hawa jamaa ni kama wako mbele ya muda ndio maana hapo kabla nikasema wanapigana vita vya kesho.

Lakini Sputanza ipo kimya. Hapo ndipo ninapolia nao hawa watu wa kuitwa Sputanza. Hawalioni hili? Hawajui kama migongano ya kichwani ni tatizo kubwa kwa wachezaji? Hawajui kama ni moja ya majukumu yao kupigania maslahi ya kiafya ya wachezaji?

PUM 02

KUHUSU SPUTANZA

Ni kifupisho cha Soccer Players' Union of Tanzania au kwa Kiswahili Umoja wa Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania.

Ni taasisi inayowakilisha wachezaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania na majukumu yake ni pamoja na kuainisha masuala mbalimbali kama hali ya maisha ya wachezaji, migogoro ya mikataba, hatua za kinidhamu na kadhalika.

Lengo mama ni kuwawakilisha wachezaji na kupigania haki na maslahi yao nchini Tanzania, huku shughuli ya uUmoja huu ni kusimamia masuala mbalimbali yanayowahusu wachezaji kama kuwapa misaada ya kisheria na matatizo ya kimikataba na kusimamia mambo ya kinidhamu.

PUM 03

Pia inaratibu matukio mbalimbali kama semina na warsha ili kuwaelimisha wachezaji. Kiongozi wa Sputanza ni Mussa Kisoki ambaye ndiye mwenyekiti wa umoja huu na ushirika wa Sputanza ni wanachama hai wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kwa picha hii niliyokupa hapa bila shaka utaona kabisa hawa jamaa wana wajibu mkubwa katika kupigania hili suala.

Ligi mbalimbali duniani zinatumia sheria hiyo, na hata kwenye mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia. Shirikisho la Soka Afrika (CAF), bado halijaanza kuitumia sheria hiyo kwenye mashindano. Lakini hiyo haina maana kwamba Tanzania pia tusiitumie kwenye mashindano yetu.

PUM 04

Sisi Tanzania kama nchi tunaweza kuitumia sheria hiyo kwa sababu ni halali na inahitajika. Kinachokosekana ni mtu wa kupeleka msukumo kwenye mamlaka za ndani za soka ili kufanya marekebisho madogo ya kanuni zao za mashindano. Na mtu huyo ni Sputanza, lakini kwa bahati mbaya imelala yoooo!