Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba wasiingie mtego wa Doumbia

DOUMBIA Pict

Muktasari:

  • Mechi hizo zote dhidi ya Mogadishu City ya Somalia na Jamus ya Sudan Kusini, zilimalizika bila Doumbia kupachika bao lakini hata Simba pia ilizimaliza kwa sare tasa.

MAMBO hayajaanza vizuri kwa Ibrahim Doumbia ndani ya Simba baada ya kuichezea katika mechi mbili za Kombe la Kagame zinazoendelea kule Rwanda.

Mechi hizo zote dhidi ya Mogadishu City ya Somalia na Jamus ya Sudan Kusini, zilimalizika bila Doumbia kupachika bao lakini hata Simba pia ilizimaliza kwa sare tasa.

Sasa baada ya hilo, kejeli zimeanza kuelekezwa kwa Doumbia kwamba Simba imepigwa na hilo linachagizwa na bao alilokosa katika mechi ya kwanza akiwa amepewa pasi nzuri na Clatous Chama ambapo aligongesha mwamba. Bahati mbaya kejeli hizo ambazo Doumbia amekuwa akipata baadhi zinatoka kwa mashabiki wa timu yake, wachambuzi kadhaa wa soka pamoja na mashabiki wa timu nyinginezo.

Ushauri wa kijiwe ni kwamba Simba wasiingie katika mtego wa kumpa presha Doumbia kisa ameshindwa kupachika bao katika mechi mbili za mwanzo ambazo ameitumikia timu au kwa bao ambalo amekosa dhidi ya Mogadishu City kwani huyo mchezaji hastahili kufanyiwa hivyo na upande wao kutokana na sababu kadhaa.

Kwanza ukiondoa nafasi ambayo alipata dhidi ya Mogadishu City, hakuna nafasi nyingine za kutosha za kueleweka ambazo Doumbia alizipata zinazotosha kumfanya abebeshwe lawama.

Cha pili, jamaa tangu asajiliwe, hajapata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake kwani baada tu ya kutanbulishwa, ameingia moja kwa kwenye timu na kuanza kuchezeshwa tena katika mashindano.

Na hilo sio kwa Doumbia tu kwani hata kwa wachezaji wengine wapya na wale ambao wameendelea kuwepo kikosini baada ya msimu uliopita ndio wametoka kwenye mapumziko ya msimu.