Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh65 milioni Goli la Mama zazaa mabao 14 timu zikivuka

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Hii ni mara ya kwanza kwa timu zote nne za Tanzania Bara kufanya hivyo tangu CAF ilipoanza kuruhusu nchi 12 Bora kwa viwango kutoa timu mbili kwenye kila shindano.

RAUNDI ya kwanza ya mechi za mchujo wa mashindano ya klabu barani Afrika imekamilika kwa timu zote nne za Tanzania Bara kufuzu raundi ya pili ya mashindano hayo ikiwa ni rekodi.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu zote nne za Tanzania Bara kufanya hivyo tangu CAF ilipoanza kuruhusu nchi 12 Bora kwa viwango kutoa timu mbili kwenye kila shindano.

Bila kudharau uwekezaji mkubwa ndani timu hizi, motisha ya GOLI LA MAMA imechangia pakubwa sana katika kuongeza hamasa kwa wachezaji. 

Mashabiki wamekuwa wakishindanisha kiwango cha pesa ambazo timu zao zinapata na kufanya kuwe na mechi mbili ndani ya moja.

Mechi dhidi ya timu pinzani uwanjani na mechi dhidi ya timu pinzani nje ya uwanja...hamasa juu ya hamasa.

Katika raundi hii Yanga ndio vinara wa kuvuna mamilioni ya mama, wakifuatiwa na Azam FC, Singida Black Stars na Simba.

Simba inaburuza mkia sio tu kwa kupata pesa kidogo baada ya kufunga mabao machache, bali pia kwa kutopata kabisa katika mechi yao ya pili ya marudiano iliyochezwa juzi Jumapili Kwa Mkapa.

Sheria ya goli la mama ni katika ushindi, sio sare wala kupoteza.

Simba hawakushinda mchezo wa mkondo wa pili kwa hiyo hawakustahili kupata, licha ya kusonga mbele.

PUM 02

Matokeo na fedha za Goli la Mama

1. Yanga SC  (5-0 Sh25 milioni)

Wiliette 0-3 Yanga

Yanga 2-0 Wiliette          


2. Azam FC (4-0 Sh20 milioni)  

El Merreikh 0-2 Azam FC

Azam FC 2-0 El Merreikh          


3. Singida BS (3-1 Sh15 milioni)

Rayon Sport 0-1 Singida BS

Singida BS 2-1 Rayon Sport                


4. Simba (2-1 Sh5 milioni)

Gaborone Utd 0-1 Simba

Simba 1-1 Gaborone Utd            

PUM 04

Raundi hii imeisha sasa inakuja raundi ijayo katikati ya Oktoba huku wapinzani wakiwa wameshajulikana kwani Yanga imepangwa kuvaana na Silver Strikers (Malawi), wakati Simba ikipangwa na Nsingizini (eSwatini).

Azam FC imepangwa na ndugu zao za visiwani, KMKM timu pekee ya Zanzibar iliyofuzu raundi ya pili na ya mwisho ya mtoano baada ya Mlandege kupoteza kwa mabao 4-3 mbele ya Insurance ya Ethiopia, huku Singida Black Stars ikipangwa sasa kukutana Flambeau du Centre ya Burundi.

Japo kwenye mpira unatakuwa kuwaheshimu wapinzani lakini hawa sio wapinzani wa kutisha sana.

Kuna uwezekano mkubwa wa timu zote nne za Tanzania kufuzu kwa hatua ya makundi msimu huu.

Na kama itakuwa hivyo basi itathibitisha zile takwimu za Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Soka (IFFHS) kwamba Ligi ya Tanzania ni namba nne kwa ubora barani Afrika.

Hatua inayokuja ni muendelezo wa vita vya kuwania mamilioni ya GOLI LA MAMA kama ilivyokuwa kwenye raundi iliyopita.

PUM 03

Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa kati ya Oktoba 17 hadi 19 na zile za mkondo wa pili kati ya Oktoba 24 hadi 26.

Baada ya hapo itafuata hatua ya makundi ambapo GOLI LA MAMA litaongezeka kutoka Sh5 milioni kwa goli moja hadi kuwa Sh10 milioni.

Sheria inabaki vile vile kwamba ili goli litoshe kuleta hela lazima timu ishinde, sio sare au ifungwe.

Katika raundi iliyopita timu zetu zilicheza kichovu kutokana na ugumu wa ratiba.

Simba na Yanga zilitoka katika mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 16 na kusafiri kwenda ugenini Kusini mwa Afrika, ilihali Singida Black Stars ilitoka kushiriki michuano ya Kombe la Kagame 2025 ambapo fainali ilifanyika Septemba 15 na timu hiyo kubeba taji mbele ya Al Hilal ya Sudan.

PUM 01

Ni Azam FC pekee ndio ilipata muda wa kutosha angalau kwa mchezo wa mkondo wa kwanza.

Hata hivyo, kwa mechi za marudiano kwa klabu zote zilikuwa na mechi za Ligi Kuu katikati yake.

Ila sasa kutakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa na kupumzika kwa raundi ijayo. Japo kuna mapumziko ya kupisha mechi za timu za taifa baada ya mechi za ligi za raundi ya tatu, ambapo Taifa Stars itacheza na Zambia kuwania kufuzu ushiriki wa Kombe la Dunia Oktoba 8.

Timu zetu zikijipanga vizuri kwa raundi ijayo na kutoboa, nchi yetu itakuwa imejiwekea historia yake katika ukanda wa CECAFA.

Mungu Ibariki Tanzania.