Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uamuzi wa kushtua! Folz abakiza wanane  

UAMUZI Pict

MASHABIKI Yanga wanalia kila kona wakiona kama mambo hayaendi vyema katika kikosi hicho, licha ya kushinda mechi zote ila soka inalocheza hawalielewi lakini kwa wachezaji wao wana raha na kocha huyo wakibaki wanane tu.

Iko hivi.  Hadi juzi kocha Romain Folz ameiongoza Yanga katika mechi zake nne za kimashindano na ni wachezaji wanane tu ambao hawajagusa nyasi za uwanja kwenye mechi za timu hiyo.

Yanga imecheza mechi nne za mashindano, ukianzia ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ikishinda 1-0, kisha ikaenda Angola katika pambano la raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete na kuondoka na ushindi mzuri wa mabao 3-0.

FOL 04

Baada ya mechi hizo mbili ikaufungua msimu wa Ligi Kuu Bara kwa kuichapa Pamba Jiji kwa mabao 3-0, kisha juzi ikamalizana na Wiliete ziliporudiana na kushinda mabao 2-0.

Katika mechi hizo nne wachezaji ambao hawakucheza hata dakika moja ni makipa Aboutwalib Mshery, Abubakar Khomeny, mabeki Abubakar Nizar ‘Ninju’, Frank Assinki na viungo Farid Mussa, Abdulnasir Mohammed ‘Casemiro’, Salum Abubakar ‘Sure boy’ na Denis Nkane.

Folz katika mechi hizo amekuwa hatabiriki akija na vikosi tofauti na rekodi zinaonyesha kila mchezo mmoja kwenda mwingine amekuwa na mabadiliko kuanzia matano hadi nane huku akiendelea kushinda.

Katika vikosi hivyo ambavyo hakuna hata kimoja kilichopoteza wala kuruhusu bao ni wachezaji wanne tu ambao ndio vinara waliocheza dakika nyingi.

Kipa Djigui Diarra ndiye namba moja akicheza mechi zote nne sawa na dakika 360, akifuatiwa na Pacome Zouzoua aliyecheza mechi zote akitumia dakika 320 kufuatia mechi mbili kutolewa kwa mabadiliko huku mwingine akiingia kipindi cha pili.

FOL 01

Kando ya Pacome yupo kiungo Aziz Andabwile ambaye ameendelea kushtua na mwanzo bora chini ya Folz akicheza muda kama huo huku Dube akifuata na beki Chadrack Boka kila mmoja akicheza dakika 310.

Rekodi zinaonyesha mbali na mechi hizo, Yanga ya Folz imecheza jumla ya mechi tisa hadi sasa zikiwamo tano za kirafiki na imefunga mabao 21 na kufungwa mawili tu, huku saba ikitoka uwanjani bila kuruhusu wavu wake kuguswa ikiwamo iley Wiki ya Mwananchi dhidi ya Bandari Kenya.

UAM 01
UAM 01

MSIKIE FERRY

Kocha wa Wiliete, Bruno Ferry akizungumzia ubora wa Yanga alisema mabingwa hao wa Tanzania msimu huu ndio wana timu kubwa zaidi kuliko msimu uliopita.

Ferry alisema kwa sasa kocha wa timu hiyo, Romain Folz anatakiwa kupunguziwa presha kwani anatengeneza kitu bora ambacho kitaibeba timu hiyo.

“Mimi sikubaliani sana na wanaoona Yanga imecheza vibaya leo (juzi) nadhani wanatakiwa kuangalia namna sisi (Wiliete) tulibadilika, mimi nimefanya kazi hapa kwangu mimi hii ndiyo timu bora,.

“Huwezi kusema hii  timu haifanyi vizuri au kocha hafai wakati anafanya mabadiliko ya wachezaji nane na bado anashinda, kiutaalam tunasema Yanga ina kikosi kipana kinachoweza kutafuta ushindi.”