Namba kwa ubora, ubora wa nini?
Haya yote ukiyaweka kwenye uhalisia wake, ligi yetu haiwezi hata kuwa
Lakini kwa maajabu ya Mungu, ni namba sita.
Ingekuwa hii nafasi ya sita imepatikana kwa kupigiwa kura, tungesema kulikuwa na uchakachuaji.
Kanuni zinazotumika kupima ubora wa ligi ni za kuunga unga sana ndio maana zinatoka na majibu kama haya.
Moja ya changamoto zinazoikabili ligi yetu na kuwafanya watu wengi kutilia shaka nafasi yake barani Afrika ni mambo rahisi sana kama miundombinu na ratiba.
Na pia yapo dunia nzima, hata kwa nchi zilizoendelea na kutumia teknolojia kubwa lakini bado waamuzi ni tatizo.
Kutoa mafunzo ya kina kwa waamuzi, au kufunga teknolojia kama VAR au GLT kunahitaji pesa nyingi, hilo tuliache.
Tuipime ligi yetu kwa vitu viwili vyepesi, miundombinu na ratiba.
Ni vyepesi kwa sababu vinahitaji maamuzi tu, wala sio pesa nyingi au maarifa makubwa sana.
Unaweza kusema kwamba miundombinu bora inahitaji uwekezaji mkubwa na uwekezaji mkubwa unahitaji pesa nyingi.
Kwa hiyo mtu anaweza kuhoji kwamba kusema kwamba yanahitajika maamuzi pekee, labda sio sahihi.
Ukweli ni kwamba ligi yetu inachezwa kwenye miundombinu mibovu sana ambayo inatumia pesa nyingi sana.
Yaani pesa inayotumika kwa miundombinu hii mibovu ingeweza kutumika nusu yake tu na kuifanya kuwa bora sana.
Achana na majukwaa, nazungumzia eneo tu la kuchezea.
Tanzania ni moja ya nchi zenye vyanzo vingi sana vya maji na mabomba ya maji yapo viwanjani na maji yanatoka.
Nyasi zinakauka, uwanja unafungiwa kisha pesa nyingi zinatumika kuukarabati.
Ukishakaa sawa, unafunguliwa nyasi hazimwagiwi, uwanja unaharibika unafungiwa tena.
Mwanza, Tabora, Mbeya, Kigoma, Dodoma na kadhalika.
Unaweza kujiuliza, huu ni mradi wa watu kwa ajili ya upigaji, au? Gharama zinatumika kufanya marekebisho ya uwanja mara kwa mara, zingetumika nusu yake tu kuimarisha mifumo ya umwagiliaji, maisha yangekuwa mepesi.
Uwanja wa Sokoine Mbeya ulifungiwa umechezewa mechi moja tu tangu ufunguliwe, Mbeya City vs Fountain Gate, tayari umeharibika.
Mechi ya Tanzania Prisons na Azam FC ilichezwa kwenye shamba la mpunga, sio uwanja.
Hapo unaweza kufungiwa tena hela ikatumika tena kufanya marekebisho,
Pata picha kwenye nchi kubwa kama Tanzania ambayo ligi inachezwa kila kona, halafu mechi ni kila baada ya siku mbili.
Machi Mosi kulikuwa na mechi moja tu ya ligi, Yanga na Simba, ambayo ilianza saa mbili usiku.
Saa 10 jioni na saa 12 jioni, ingewezekana kukawa na mechi zingine, lakini hawakuweka, badala yake mechi zote zikawa Machi 2.
Halafu timu zilizocheza siku hiyo, zikawa na mechi nyingine Machi 5.
Ilicheza Machi mbili dhidi ya Pamba, mjini Mwanza halafu ikacheza na TZ Prisons Machi tano mjini Mbeya.
Maana yake baada ya mechi ya Machi pili, kukawa na safari ya kutoka Mwanza kwenda Mbeya.
Ok, tuseme hawa ni Azam, watoto wa Bakhresa, mtu mwenye pesa zake kwa hiyo watapanda ndege.
Hakuna ndege ya moja kwa moja kutoka Mwanza kwenda Mbeya ni hadi ufike Dar es Saalam na kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ndege ni moja tu kwa siku, saa kumi jioni.
Kwa hiyo baada ya mechi, Machi pili wakasafiri Machi tatu hadi Dar es Salaam na jioni wakapanda ndege kwenda Mbeya.
Hiyo siku imekufa bila mazoezi wanafika Mbeya na kufanya mazoezi ya siku moja, kesho yake mechi.
Kwa utaratibu wa sayansi ya michezo, ni muhimu sana kufanya mazoezi ya kurudisha mwili kwenye hali ya kawaida (recovery), siku moja baada ya mechi, hawakupata nafasi.
Kwanini ile mechi ya Machi 2 isingechezwa Machi Mosi saa kumi jioni, halafu Machi 2 wakapata muda mzuri wa kurudisha miili katika hali ya kawaida, na Machi tatu wakasafiri kwa utulivu?
Kuliona hili inahitaji pesa kiasi gani kuliona? Machi 19, Kigoma na Machi 22 Singida.
Kwa barabara huu ni umbali wa zaidi ya kilomita 700, safari ya zaidi ya saa 10 barabarani.
Singida hakuna uwanja wa ndege, hivyo kama ndege itatumika, basi ni hadi Dodoma.
Kutoka hapo ni kwa basi maana yake hiyo ni Machi 20, siku inakufa hivyo, bila kurudisha miili ya wachezaji katika hali ya kawaida.
Na ratiba ya aina hii sio Azam tu, ni kwa timu zote.
Haya, Azam, Simba na Yanga wanaweza kuwa na jeuri ya kupanda ndege, vipi hawa wengine, wenzangu na mimi?
Lakini wakati maeneo mengine yakiboresheka, miundombinu na ratiba imebaki palepale.
Iamuliwe tu kwamba ligi itachezwa KMC Complex, Azam Complex, Meja Isamuhyo, Aman Complex na Gombani tu, basi.
Hakuna uwanja wa kufanyiwa marekebisho kati ya Mwanza, Dodoma, Mbeya, Tabora na Kigoma.