Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Man United awavuta Wabongo England

NYOTA Pict


KATIKA ulimwengu wa soka wa Kiafrika ndoto za vijana wengi huanzia kwenye viwanja vya vumbi huko mitaani tena katika familia za hali ya chini na hata shule za kawaida ambazo miundombinu ya kisasa ni kitendawili.


Lakini kwa bahati nzuri, mara nyingine ndoto hizo hupata watu, taasisi na fursa zinazoweza kuzigeuza kuwa uhalisia.


Hivi ndivyo ilivyotokea kwa wachezaji wawili chipukizi kutoka Tanzania Mwakipesile Gwakisa aliyezaliwa Juni 24, 2010 na Calvin Emanuel Oktoba 22, 2009 ambao wamepata mwaliko maalumu kwenda England kushiriki katika mpango wa maendeleo ya soka inayoendeshwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Febian Brandy.

Wachezaji hao wawili wapo chini ya usimamizi wa taasisi ya AYE (African Youth Empowerment), taasisi ambayo imejikita katika kutambua, kukuza na kusimamia vipaji vya vijana wa Kiafrika, hususani wale wa Kitanzania kwa kuwaandaa kupata fursa ndani na nje ya nchi.

NYO 01

BRANDY NI NANI

Febian Brandy ni mmoja wa wachezaji waliowahi kutabiriwa kufanya makubwa kwa miaka ya baadae katika soka la England. Akiwa na kasi ubunifu na uwezo wa kucheza nafasi ya mshambuliaji au winga, Brandy alijiunga na akademi ya Manchester United akiwa na miaka tisa hatua ambayo ni ndoto ya vijana wengi duniani.

Alipata nafasi ya kufanya mazoezi bega kwa bega na nyota wakubwa waliota mizizi klabuni hapo, chini ya makocha waliotengeneza vizazi vya wachezaji bora barani Ulaya. Hata hivyo, majeraha na ushindani mkali baada ya kukomaa tayari kwa soka la ushindani vilimfanya asidumu kwa muda mrefu katika kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Baada ya hapo, alizizunguka klabu mbalimbali ndani na nje ya England kabla ya hatimaye kustaafu. Lakini kama ilivyo kwa wanamichezo wengi wenye maono, Brandy hakuuona mwisho wa maisha yake ya soka uwanjani kuwa mwisho wa mchango wake kwa mchezo huo.

Badala yake, aliamua kuutumia uzoefu wake kuwawezesha vijana wengine wasipitie alichopitia  bali wapate mwongozo mapema na msaada wa kitaalamu.

Hapo ndipo akazindua mradi unaojulikana kama skouted pamoja na programu (aplikesheni) na timu mbalimbali za vijana (ikiwemo Skouted FC), ambazo lengo lake ni kuvumbua vipaji vilivyofichika duniani kote na kuwapa fursa ya kuonekana na kuunganishwa na klabu na akademi kubwa.

Sasa kupitia ushirikiano wake na taasisi ya AYE, macho yake yameangukia Afrika na Tanzania nayo imo katika ramani hiyo.

NYO 02

SAFARI ILIVYO

Taasisi ya AYE imejijengea jina ndani na nje ya Tanzania kwa juhudi zake za muda mrefu katika kusimamia na kuendeleza vipaji vya vijana. Kupitia programu zake, imewahi kuwaunganisha wachezaji kadhaa na majaribio (trials), akademi za kimataifa na mashindano mbalimbali nje ya nchi.

Akizungumzia fursa iliyopatikana kwa Mwakipesile na Calvin mkurugenzi wa AYE, Gerald Muyimba  anasema: “Tulipoanza AYE lengo letu kuu lilikuwa ni kufungua milango kwa vipaji vilivyokuwa vinaishia mtaani kwa kukosa msaada. Febian Brandy ameona kazi tunayofanya, ameona ubora wa vijana wetu, ndipo akaamua kuwapa nafasi hii. Hii ni fursa adimu kwa vijana hawa na kwa Tanzania kwa ujumla.”

Anaongeza kuwa mchakato wa kuwapendekeza wachezaji hao haukuwa wa kubahatisha, bali ulitokana na tathmini ya kina ya uwezo wao, nidhamu na  kasi ya kujifunza.

NYO 03

MADOGO WAFUNGUKA

Akizungumza kuhusu mwaliko wa kwenda England, Mwakipesile ambaye ana umri wa miaka 14 anayependa kucheza kiungo na wakati mwingine winga anasema: “Niliposikia kuhusu hii safari, niliona kama naota. Manchester United ndio timu niliyokuwa nikiifuatilia tangu nikiwa mdogo. Sasa mtu aliyekuwa pale ananitaka niende England kwa ajili ya kuendeleza kipaji changu… ni jambo kubwa sana kwangu na familia yangu.”

Kwa upande wake, Calvin mwenye umri wa miaka 15 ambaye anamudu kucheza winga zote mbili anasema: “Ninamshukuru Mungu, AYE, na watu wote walioniunga mkono. Hii ni nafasi niliyokuwa naota kila siku. Kwenda England chini ya mtu aliyekuwa Manchester United ni heshima kubwa.”

NYO 04

BRANDY MWENYEWE

Akizungumzia uamuzi wake wa kuwachagua vijana hao kutoka Tanzania, Febian Brandy anasema: “Nimeona vipaji vingi duniani, lakini kuna kitu maalumu nilikiona kwa hawa vijana wawili hivyo nikaona sio mbaya waje tuwatazame kwa karibu na kuona nini kikubwa tufanye kwa ajili yao.”

Anaongeza kwa kusema, “hatutaki tu kuwafanya wawe wachezaji bora, tunataka wawasaidie kuwa watu bora wenye nidhamu, maono na malengo. England watapata mafunzo ya kiwango cha juu, watajifunza mbinu, akili ya mchezo na mazingira ya ushindani ya kweli.”

Kwa mujibu wa Brandy, lengo la muda mrefu ni kuona vijana wengi zaidi kutoka Afrika wakipata nafasi katika soka la kulipwa barani Ulaya na duniani kwa ujumla.

NYO 05

MAANA YAKE KWA TANZANIA

Mwaliko wa wachezaji hawa wawili sio mafanikio yao binafsi pamoja na taasisi wa AYE, bali ni hatua muhimu kwa maendeleo ya soka la vijana nchini. Ni ishara kuwa macho ya dunia yanaanza kuangalia vipaji vilivyopo mitaani, shuleni na kwenye akademi ndogo. Ni uthibitisho kuwa kwa mfumo mzuri, usimamizi sahihi na kujituma, kijana wa Kitanzania anaweza kufika mbali bila kujali alipoanzia.

Safari ya Mwakipesile na Mushi kwenda England ni mwanzo wa ukurasa mpya kwa kizazi hiki cha vijana wanaoota kuwa wanasoka wa kulipwa.