Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Arteta asherehekea ushindi wa kihistoria Anfield

SHEREHE Pict

Muktasari:

  • Arsenal ilifanya sherehe za ushindi kwa furaha kubwa ndani ya Uwanja wa Anfield. Mwisho wa mchezo baina ya timu hizo, kocha Mikel Arteta aliruka na kumkumbatia kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Gabriel Heinze, akisherehekea ushindi wake wa kwanza dhidi ya Liverpool akiwa kocha wa Arsenal, ushindi wa kwanza wa klabu hiyo ugenini Anfield katika Ligi Kuu England ndani ya miaka 14 na pia kuifanya timu yake, ambayo ni mabingwa watetezi kuongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tatu.

LIVERPOOL, ENGLAND: ANDONI Iraola alipuuzia maswali yoyote yaliyohusisha uwezo wa Liverpool kutwaa ubingwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, akijibu kwa maneno mawili rahisi tu.”Bado mapema,”  alikuwa akijibu kila alipoulizwa.

Kocha huyo mkuu wa Liverpool alionyesha kutokuwa tayari kujadili suala hilo kwa kuzingatia hatua ya msimu ilipofikia, lakini kama Arsenal ilivyoonyesha kwa vitendo kwa kupambana kwa nguvu, kauli ya kwamba bado ni mapema pia inahusu maendeleo ya kikosi chake.

Arsenal ilifanya sherehe za ushindi kwa furaha kubwa ndani ya Uwanja wa Anfield. Mwisho wa mchezo baina ya timu hizo, kocha Mikel Arteta aliruka na kumkumbatia kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Gabriel Heinze, akisherehekea ushindi wake wa kwanza dhidi ya Liverpool akiwa kocha wa Arsenal, ushindi wa kwanza wa klabu hiyo ugenini Anfield katika Ligi Kuu England ndani ya miaka 14 na pia kuifanya timu yake, ambayo ni mabingwa watetezi kuongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tatu.

Wachezaji wake, ambao walipambana bila kuchoka kuhakikisha wanalinda bao la mapema la Kai Havertz, walipanga foleni kupokea pongezi kutoka kwa mashabiki wao waliokuwa na furaha katika jukwaa la wageni. Hasira zilitawala sehemu nyingine za uwanja.

SHERE 04

MAMBO MAGUMU

Kuanzia beki Virgil van Dijk kuonyeshwa kadi ya njano baada ya mchezo kwa kumshangilia mwamuzi Andy Madley kwa kejeli, hadi mashabiki wa nyumbani kuwazomea waamuzi wa mchezo kwa hasira, lakini zaidi wakikasirishwa na mbinu za Arsenal za kutumia uzoefu na ujanja wa kucheza ili kupata matokeo (au vitendo vya kucheza rafu na kupoteza muda, kutegemea mtazamo), ulikuwa usiku wenye kukatisha tamaa kwa timu iliyokuwa imeingia uwanjani ikiwa na mwendelezo mzuri wa matokeo na kukiwa na mazungumzo kuhusu uwezekano wa kuwania ubingwa.

Wachezaji wa Liverpool walipoondoka uwanjani walipigiwa makofi pekee, mashabiki wakitambua juhudi zao na bahati mbaya iliyowakumba.

Timu hiyo nyumbani ilipaswa kupata penalti baada ya Jurrien Timber kuvuta jezi ya Alexander Isak na kumzuia asiucheze mpira uliokuwa ukipigwa na Bradley Barcola.

Florian Wirtz alipiga mpira uliogonga mwamba wa juu wa lango wakati Liverpool ilipokuwa katika kipindi chake bora zaidi cha mchezo, huku Alexis Mac Allister akipoteza nafasi nzuri ya kufunga kwa kichwa akiwa umbali wa mita 12 kutoka langoni.

Hata hivyo, kadiri kipindi cha pili kilivyoendelea na Arsenal kuhimili mashambulizi ya Liverpool, huku Gabriel Magalhaes na Declan Rice wakiongoza safu ya ulinzi, matumaini ya Liverpool ya kurejea mchezoni yalizidi kupungua. Hakukuwa na ishara iliyoonyesha wazi zaidi namna timu iliyokusanya wachezaji wa gharama kubwa ilivyokosa mawazo mapya ya kushambulia kama kumuona Van Dijk akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati kwa muda katika dakika za mwisho za mchezo.

SHERE 03

Van Dijk alikuwa na Isak, Barcola na wachezaji walioingia kama mbadala, Lewis Koumas, Victor Muñoz na Rio Ngumoha, waliokuwa wakimsaidia. Ngumoha alionyesha mchango fulani, lakini kwa ujumla safu ya ushambuliaji ya Liverpool iliyokuwa na wachezaji wa aina mbalimbali haikuweza kuleta matokeo bora.

Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 16, Liverpool ilimaliza mchezo wa Ligi Kuu England bila kupiga hata shuti moja lililolenga lango. Malalamiko ya Iraola kwamba vipigo viwili vya Liverpool msimu huu vilichangiwa na uamuzi wenye utata wa waamuzi yalikuwa na msingi. Hata hivyo, alimaliza mjadala huo kwa kutoa hoja muhimu.

“Nadhani ilikuwa penalti, lakini tunahitaji kufikiria mambo tunayoweza kuboresha ili kuwa upande sahihi katika michezo mikubwa kama hii,”  alisema Iraola.

SHERE 01

MWANZO WA AJABU

Mwanzo mwingine wa taratibu uliigharimu Liverpool, lakini pia ilikosa makali ya kushambulia na uimara wa ulinzi ambao uliiwezesha Arsenal kupata ushindi huo. Mambo hayo yatakuja kadiri muda utakavyopita chini ya Iraola. Kwa sasa, kutakuwa na somo gumu ambalo wakati mwingine italazimika kukubali na kujifunza kutokana nalo.

Iraola alionyesha kuwa yupo tayari kuwaamini na kuwapa nafasi wachezaji vijana wenye vipaji baada ya kumpa Trey Nyoni nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza kwenye Ligi Kuu England.

Ulikuwa uamuzi wa ujasiri kutoka kwa kocha huyo ambaye alimwacha Ryan Gravenberch benchi pamoja na Dominik Szoboszlai aliyekuwa amerejea baada ya kupona jeraha, ili kumpa nafasi kijana huyo mwenye umri wa miaka 19. Hata hivyo, uamuzi huo ulitokana na uwezo aliouo nyesha mche zaji huyo.

SHERE 02

Nyoni alikuwa amemvutia Iraola tangu alipojiunga na klabu hiyo majira ya kiangazi na akaongeza kiwango chake wakati wa ziara ya maandalizi ya msimu ya Liverpool nchini Marekani. Ilikuwa ni wazi kwamba mchezo wake wa kwanza ulikuwa unakaribia, na uamuzi wa kumpa nafasi hiyo katika mchezo dhidi ya mpinzani mwenye nguvu kubwa kama Arsenal uliongeza uzito wa imani ambayo kocha alikuwa nayo kwake.

Nyoni alionyesha uwepo wake uwanjani mara moja. Moja ya mashaka kuhusu kumchezesha kiungo huyo dhidi ya safu ya kiungo ya Arsenal iliyokuwa na Rice, Bruno Guimarães na Martin Odegaard ilikuwa kama alikuwa na nguvu za kutosha za kimwili kushindana nao. Hata hivyo, baada ya sekunde 49 pekee, alimwangusha Odegaard na kusababisha mpira wa adhabu wa kwanza wa mchezo huo.

Dakika ya 10, alimchezea Havertz rafu kwa kuchelewa na kukanyaga sehemu ya kifundo cha mguu wake. Huenda alikuwa na bahati ya kutoonyeshwa kadi ya kwanza ya njano katika mchezo huo.

SHERE 05

Nyoni alionyesha usahihi zaidi katika muda wa kukutana na mpira, kasi na nguvu zake zilionekana wazi alipomzidi Odegaard katika pambano la kuwania mpira, wakati wachezaji hao walipokuwa wakikimbilia kuupokea mpira uliokuwa umetolewa na kipa David Raya.


MWAMUZI VIPI?

Arsenal iliokoka kwa haki baada ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) kufanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa penalti dhidi ya Christos Tzolis katika kipindi cha mashambulizi makali yaliyofuatia hatua ya Nyoni kutembea na mpira.

Utulivu wa kijana huyo anapokuwa na mpira na uwezo wake wa kusoma mchezo vilikuwa mambo yaliyotia moyo zaidi kwenye mchezo wake wa kwanza kucheza dakika zote za kawaida za ligi.

Hata hivyo, kilichomkwamisha mchezaji huyo ni hitaji la Liverpool la kutafuta bao la kusawazisha tangu dakika ya 16 ya mchezo. Iraola alihitaji nguvu zaidi za kushambulia na kuleta vurugu katika eneo la mwisho la uwanja kuliko mchango wa kijana huyo katika kulinda safu ya kiungo na kujenga mashambulizi kwa utulivu.

SHERE 05

Hivyo kutolewa kwake na nafasi yake kuchukuliwa na Szoboszlai dakika ya 59 kulitokana na mazingira ya mchezo, siyo kwa sababu ya mchango wake binafsi. Hata hivyo, Liverpool ilionyesha vurugu nyingi lakini haikuwa na mpangilio katika mashambulizi ya mwisho.

Licha ya hasira zilizokuwepo kuhusu vitendo vya Gabriel, Havertz na uamuzi wa mwamuzi Madley, kulikuwa na tofauti ya kiwango kati ya mabingwa na timu zinazotajwa kuwa zinaweza kuwania ubingwa. Bado mapema, kama Iraola alivyosema. Lakini wapewe muda.