Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo yanayoweza kuwa hatari kwa afya yako

UREMBO Pict

Muktasari:

  • Tafiti za hivi karibuni zinaendelea kuonyesha umuhimu wa mtindo bora wa maisha katika kuzuia magonjwa sugu. Hizi ni starehe tano zinazohitaji udhibiti ili kulinda afya.

Wakati wengi wakitafuta furaha kupitia burudani, vyakula wanavyovipenda na muda wa kupumzika, baadhi ya starehe hizo zinaweza kugeuka kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.

Kuanzia kunywa pombe na kuvuta sigara hadi kukesha na kula vyakula visivyo na virutubisho vya kutosha, wataalamu wanaonya kuwa mazoea yanayojirudia yanaweza kuathiri afya taratibu bila mtu kutambua.

Tafiti za hivi karibuni zinaendelea kuonyesha umuhimu wa mtindo bora wa maisha katika kuzuia magonjwa sugu. Hizi ni starehe tano zinazohitaji udhibiti ili kulinda afya.


URE 04

1. KUNYWA POMBE KUPITA KIASI

Kwa baadhi ya watu, pombe ni sehemu ya sherehe, mikusanyiko ya marafiki na mapumziko baada ya kazi. Hata hivyo, matumizi yake yanaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya ini, moyo na saratani mbalimbali.

Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya Juni 2024 ilieleza kuwa takribani vifo milioni 2.6 duniani mwaka 2019 vilihusishwa na matumizi ya pombe. WHO pia inabainisha kuwa pombe inahusishwa na zaidi ya magonjwa na hali nyingine 200. Ushahidi huo unaonyesha kuwa unywaji wa pombe si suala la burudani pekee, bali pia ni changamoto ya afya ya umma.

Daktari wa binadamu Dorcas Natse anasema kuwa; “Kupunguza au kuacha pombe husaidia kupunguza hatari zake, akuna kiwango cha pombe kinachoweza kuhakikishwa kuwa hakina hatari kabisa, hasa kuhusiana na saratani.”


URE 02

2. KUVUTA SIGARA, SHISHA

Sigara na shisha hutumiwa na baadhi ya watu kama njia ya kujifurahisha au kushirikiana na marafiki. Hata hivyo, moshi wake una kemikali hatari zinazoweza kuharibu mapafu na mishipa ya damu. Matumizi ya tumbaku huongeza hatari ya saratani, magonjwa ya moyo na kiharusi.

WHO inaeleza katika taarifa yake ya mwaka 2025 kuhusu udhibiti wa tumbaku kwamba matumizi ya tumbaku yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya duniani. Ripoti hiyo inasisitiza umuhimu wa kuwaelimisha watu kuhusu madhara ya tumbaku na kuwasaidia wanaotaka kuacha.

Daktari Natse anasema; “Uvutaji wa sigara hauathiri mvutaji pekee. Moshi wake unaweza kuwaathiri pia watu wanaokaa karibu naye, wakiwamo watoto.”


URE 03

3. KUKAA BILA MAZOEZI

Kutazama televisheni, kutumia simu kwa muda mrefu na kukaa bila kufanya shughuli za mwili kunaweza kuonekana kuwa mapumziko yasiyo na madhara, kutofanya mazoezi ya kutosha kunaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo, kisukari aina ya pili na unene uliopitiliza.

WHO, katika taarifa yake ya Juni 2024, ilikadiria kuwa asilimia 31 ya watu wazima duniani, sawa na takribani watu bilioni 1.8, hawakufikia kiwango kinachopendekezwa cha mazoezi mwaka 2022. Shirika hilo linashauri watu wazima kufanya mazoezi ya wastani kwa dakika 150 hadi 300 kwa wiki.

Kutembea kwa kasi, kucheza dansi, kuendesha baiskeli na kufanya kazi za nyumbani ni njia zinazoweza kusaidia kuongeza mwendo wa mwili.


URE 01

4. MUDA WA KULALA

Kukesha kwa ajili ya burudani, simu au mitandao ya kijamii kunaweza kuathiri afya kunapokuwa mazoea. Usingizi usiotosha unaweza kupunguza umakini, kuathiri hisia na kuhusishwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.

Vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa vya Marekani (CDC), katika taarifa ya Mei 2024, vinaeleza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 18 hadi 60 wanahitaji kulala angalau saa saba kila usiku.


URE 05

5. KULA VYAKULA VYENYE MAFUTA, CHUMVI NA SUKARI NYINGI

Vyakula vya haraka, vitafunwa na vinywaji vyenye sukari nyingi vinaweza kufurahisha ulimi, lakini vikiliwa mara kwa mara bila uwiano vinaweza kuchangia matatizo ya kiafya.

Ulaji wa chumvi nyingi huongeza hatari ya shinikizo la juu la damu, huku ulaji wa sukari nyingi ukichangia kuongezeka kwa uzito na hatari ya matatizo ya kimetaboliki.

WHO inaeleza kuwa ulaji wa chumvi kwa watu wazima unapaswa kuwa chini ya gramu tano kwa siku. Pia inapendekeza watu wenye umri wa zaidi ya miaka 10 kula angalau gramu 400 za matunda na mboga kwa siku.