Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa ratiba hii... Muda wa kupumzika kwa wachezaji ni mtihani

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, ratiba hiyo inaonyesha kuna changamoto ya muda hasa kwa timu kusafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine na mapumziko ya wachezaji, jambo ambao kama umakini ungezingatiwa hayo yangeepukika.

BODI ya Ligi Kuu Bara (TPLB) imetoa ratiba ya msimu wa 2025-2026 uliopangwa kuanza Septemba 17 kwa mechi mbili - KMC itacheza na Dodoma Jiji, Dar es Salaam ilhali Coastal Union dhidi ya Tanzania Prisons uwanjani Mkwakwani, Tanga, ikiwa ni siku moja baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii, Septemba 16.

Hata hivyo, ratiba hiyo inaonyesha kuna changamoto ya muda hasa kwa timu kusafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine na mapumziko ya wachezaji, jambo ambao kama umakini ungezingatiwa hayo yangeepukika.

Mfano ni mechi mbili za mwanzo za Dodoma Jiji. Walima zabibu hao watakuwa ugenini Septemba 17 dhidi ya KMC na Septemba 20 watasafiri hadi Tabora kucheza na Tabora United.

Hii maana yake ni baada ya mchezo na KMC Septemba 18 itatakiwa kusafiri kisha Septemba 19 ifanye mazoezi ya kurudisha miili kwenye hali yake ya kawaida kwa sababu ya uchovu wa mechi ya Septemba 17 na safari ya takriban saa 15, na Septemba 20 icheze.

Kiufundi hilo siyo sawa kwa sababu itakosa siku ya kufanya mazoezi ya kimbinu kwa ajili ya mchezo wenyewe na ni wazi ingetakiwa ipate siku moja zaidi yaani mechi ichezwe Septemba 21, kama Tanzania Prisons ambao watafungua msimu ugenini dhidi ya Coastal Union Septemba 17 na mechi ijayo itacheza ugenini Septemba 21 dhidi ya Namungo.

PUM 01

Dodoma Jiji itabanwa na muda wa maandalizi kuliko Prisons ilhali wao ndiyo wana safari ndefu zaidi. Kwa hiyo italazimika kufanya kimoja kati ya yafuatayo ili icheze mechi hiyo:

Mosi, kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Yaani Septemba 19 ifanye mazoezi ya kurudisha miili katika hali ya kawaida halafu papo hapo ifanye mazoezi ya mbinu kwa ajili ya mchezo.

Hata hivyo hii siyo sawa na sahihi kwa faida ya mpira. Wachezaji watakuwa na uchovu kiasi kwamba miili yao haitafunguka vya kutosha kwa ajili ya kupokea mazoezi. Matokeo yake mchezo utapooza na kukosa ushindani.

Pili, kusafiri baada ya tu mechi Septemba 17. Japo hii ndiyo njia ambayo timu nyingi hutumia kutokana na mazingira ye kivyetu vyetu, lakini nayo siyo sawa na sahihi.

Usafiri ambao timu nyigi hutumia siyo rafiki kwa wanamichezo. Mabasi zinayotumia na viti vyake - kwa safari ya saa 10 na kuendelea, miguu lazima ivimbe.

Kwa mchezaji ambaye ametoka katika mechi ngumu safari za aina hiyo ni sawa na mechi nyingine na matokeo yake mechi inayofuata haiwezi kuwa na ushindani unaostahili.

PUM 02

Hapo bado kuna mechi nyingi hazijapangiwa tarehe - zinaweza kupangwa humohumo ikawa balaa zaidi.

Maana yake kuna uwezekano mkubwa hizo siku za kupumzika, kusafiri na kujiandaa zikapungua zaidi na zaidi.

Na kama itakuwa hivyo, basi muda wa wachezaji kupumzika utakuwa mdogo zaidi.

Wachezaji wasipopumzika vya kutosha maana yake hawatakuwa na nguvu za kutosha kutoa kinachotarajiwa kwenye ligi na hata kwenye timu ya taifa.

Timu ya taifa inategemea wachezaji wengi wanaocheza nyumbani. Wanapochoshwa namna hiyo hawawezi kuwa na nguvu za kushindana barabara na matokeo yake Madagascar ambako ligi yao ni dhaifu wameishangaza Afrika kwenye CHAN 2024 kuliko wenyeji wenye ligi namba nne kwa ubora Afrika.

PUM 03

Uliwaangalia Madagascar wanavyocheza, utapenda - hawachoki. Muda unavyozidi kwenda ndivyo wanavyozidi kuwa na nguvu.

Hiyo huwezi kuiona kwa Stars -ilipocheza nao walionyesha udhaifu wa Stars. Japo waliwafunga lakini Stars iliteseka. Ratiba ya ligi izingatie muda wa wachezaji kupumzika baada ya mechi na safari.

Nchi ni kubwa na timu zimetawanyika. Timu itoke Kigoma iende Tanga halafu Mbeya - si mchezo.

Msimu uliopita Azam ilicheza Mbeya Aprili 3 dhidi ya KenGold ikaenda Singida kucheza Aprili 6 dhidi ya Black Stars na kisha Aprili 9 ikacheza na Yanga jijini Dar es Salaam.

Unaweza kusema Azam wana uwezo kwa hiyo watapanda ndege, lakini Singida hakuna uwanja.

Labda watashukia Dodoma halafu waende na basi, lakini hata hivyo hakuna ndege ya kutoka Mbeya kwenda Dodoma.

Kwa hiyo safari ya Mbeya kwa Singida Black Stars kwa vyovyote ni siku mbili.

PUM 04

Mechi ni Aprili 6 - safari siku mbili yaani Aprili 7 na 8 - mechi Aprili 9.

Hakuna muda wa kupumzika. Hakuna muda wa kurejesha mwili kwenye hali ya kawaida. Halafu papo hapo kuna mechi ya Yanga. Inawezekanaje.

Msimu mmoja nyuma yake yaani 2023-2024 Kagera Sugar ilianza ligi mjini Kigoma dhidi ya Mashujaa Agosti 16, 2023.

Siku tatu baadaye yaani Agosti 19 ikawa na mechi dhidi ya Ihefu huko Mbalali Mbeya. Safari ya Kigoma hadi Mbeya ni siku mbili njiani. Ikafikia uwanjani na kufungwa.

Hakuna kudanganyana na saa 72 za Fifa kutoka mchezo mmoja kwenda mwingine. Tanzania na Bodi ya Ligi tupo kwenye mazingira tofauti.

Safari ndefu kwenye mabasi magumu, njia za kizamani za kurejesha miili kwenye hali ya kawaida, lishe duni na hata tiba za kuunga unga ndiyo maisha ya kawaida.

Ni vyema kuondoa hii changamoto ya kubana siku za kupumzika. Inatesa wachezaji na kuihujumu timu ya taifa.