Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia U-17 lilivyogeuka soko la vipaji Ulaya

VIJANA Pict

Muktasari:

  • Klabu kubwa duniani hazisubiri mchezaji afikishe umri wa kucheza timu ya wakubwa ndipo zianze kumfuatilia. Zinawekeza katika mifumo ya kutambua na kukuza vipaji tangu umri mdogo, huku mashindano ya kimataifa ya vijana yakiwa sehemu muhimu ya kufanya tathmini.

ACHANA na ushindani unaoonyeshwa na mataifa mbalimbali kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la vijana U-17 yanayoendelea Qatar, jukwaa hilo limegeuka kuwa soko la vipaji kwa klabu kubwa duniani, hasa za Ulaya zinazotafuta nyota wa baadaye.

Hata kabla ya michuano hiyo kuanza Novemba 19, 2026, baadhi ya vijana waliokuwa wakishiriki mashindano ya kufuzu walikuwa tayari wamevutia maskauti na klabu zenye majina makubwa.

Klabu kubwa duniani hazisubiri mchezaji afikishe umri wa kucheza timu ya wakubwa ndipo zianze kumfuatilia. Zinawekeza katika mifumo ya kutambua na kukuza vipaji tangu umri mdogo, huku mashindano ya kimataifa ya vijana yakiwa sehemu muhimu ya kufanya tathmini.

Qatar imewakutanisha vijana kutoka mataifa 48, hivyo kila mchezo ni nafasi ya kuongeza thamani ya mchezaji na kuonyesha uwezo mbele ya wadau wa soka.


VIJA 01

ISSA CHOLE (TANZANIA)

Chole tayari alikuwa amegeuka gumzo kwenye soko la vipaji kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia. Baada ya kuiongoza Serengeti Boys hadi fainali ya AFCON U-17 nchini Morocco mwaka 2026 na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano hayo, aliingia kwenye rada za klabu kadhaa za Ulaya.

Olympique Marseille ya Ufaransa iliripotiwa kumfuatilia, huku SK Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech ikitajwa kuwasilisha ofa ya takribani Dola 190,000 (Sh507 milioni za Tanzania).

Klabu nyingine zilizohusishwa na nia ya kumtaka ni Como 1907 ya Italia, FC Metz (Ufaransa), Malmö FF na BK Hacken zote za Sweden.


VIJA 02

EDWIN NA HOLGER QUINTERO (ECUADOR)

Edwin na Holger Quintero, tayari wamepata nafasi ya kujiunga na Arsenal. Klabu hiyo ya England ilitangaza makubaliano ya kuwasajili mapacha hao kutoka Independiente del Valle, huku wakitarajiwa kujiunga rasmi Agosti 2027 watakapofikisha miaka 18.

Edwin ni winga mwenye kasi na uwezo wa kupambana na mabeki mmoja kwa mmoja, wakati Holger ni kiungo mshambuliaji mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi. Hawa ni mfano wa wachezaji ambao safari yao kuelekea klabu kubwa imeanza kabla ya Kombe la Dunia.


VIJA 03

SAMUEL MARTINEZ (COLOMBIA)

Martinez alivutia klabu za Ulaya kupitia kiwango chake katika mashindano ya kufuzu ya Amerika Kusini.

Kiungo huyo wa Atletico Nacional alisaidia Colombia kutwaa ubingwa wa Amerika Kusini U-17 mwaka 2026, mafanikio yaliyomuwezesha kuivutia Liverpool.

Klabu hiyo ilikubaliana kumsajili baada ya kuwania saini yake na Manchester City, Bayern Munich na Borussia Dortmund, huku akitarajiwa kujiunga nayo msimu wa 2027-2028. Hii inaonyesha jinsi mashindano ya vijana yanavyoweza kuwa daraja la kukuza vipaji.


VIJA 04

SIMON ESCOBAR (ARGENTINA)

Escobar ambaye ni beki wa kushoto wa Vélez Sarsfield, amekuwa akifuatiliwa na klabu za England, zikiwemo Chelsea na Brighton.

Uwezo wake wa kusaidia mashambulizi na kucheza kwa ujasiri katika nafasi ya beki umemfanya kuwa miongoni mwa vijana wanaovutia macho ya maskauti.


VIJA 05

EDUARDO CONCEICAO (BRAZIL)

Wakati huo huo, Conceicao anayekuzwa na akademi ya Palmeiras, anatajwa kuwavutia Barcelona, Paris Saint-Germain, Chelsea, Manchester United na Manchester City.

Inaelezwa bado Conceicao hajakubaliana na klabu hizo ingawa zote zimemfuatilia, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa atakachokifanya kwenye Kombe la Dunia kikampa dili kwenye moja ya timu hizo.


VIJA 06

CHEIKH DIENG (SENEGAL)

Beki wa Senegal, Cheikh Dieng, anayekipiga Diambars FC, tayari ameripotiwa kuvutia klabu za Ulaya na kufanya majaribio katika Anderlecht ya Ubelgiji.