Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kila mmoja awalinde madogo Serengeti Boys

SERENGETI Pict

Muktasari:

  • Boli linatembea kinoma na timu pinzani zinausaka kwa tochi japo ndiyo hivyo tena matokeo hayajawa mazuri katika mechi mbili ambazo tumeshacheza.

SERENGETI Boys wanapiga mpira mkubwa sana kule Qatar kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.

Boli linatembea kinoma na timu pinzani zinausaka kwa tochi japo ndiyo hivyo tena matokeo hayajawa mazuri katika mechi mbili ambazo tumeshacheza.

Fikiria timu kama Brazil ambayo ina uzoefu mkubwa na mashindano ya vijana na imekuwa na mifumo bora ya kukuza vipaji, wachezaji wao wanatoa machozi ya furaha baada ya mechi kisa wameshinda bao 1-0 na Tanzania.

Na hilo boli, Serengeti Boys walianza kulitembeza tangu walipokuwa kule Morocco kwenye fainali za Mataifa ya Afrika.

Sasa kwa vile madogo anaonyesha mwanga mzuri wa kubeba taifa kisoka hapo baadaye, tunapaswa kuwalinda kwa nguvu na gharama zote ili tunachokitamani kije kutimia.

Kila mmoja wetu anapaswa kubeba dhamana ya kuhakikisha Serengeti Boys hii ndio inakuwa timu bora ya Taifa ya wakubwa ya Tanzania hapo baadaye.

Klabu zinazowamiliki hao wachezaji hazitakiwi kuleta tamaa pale zitakapokuja ofa za klabu za Ulaya kwa ajili ya kuwasajili watoto hao.

Wazazi hawatakiwi kuingia tamaa ya kushawishika na fedha za klabu za hapa Tanzania zitakazowahitaji watoto hao na kuzuia mipango ya kwenda nje.

Na sisi wengine tunatakiwa kuwalinda wachezaji hao dhidi ya majaribio yoyote yale ambayo hayaonekani kuwa na mlengo mzuri kwa maendeleo ya vijana wetu hao.