Kazimoto anavyopiga kazi mbele ya Kibwana, Mwenda
Muktasari:
- Kiwango alichokionyesha beki huyo ni kama anatuma ujumbe wa kuamsha ushindani kwenye kikosi cha Yanga ambacho kina mabeki wanne, Kibwana Shomari, Israel Mwenda na Yao Attohoula ambaye amekuwa akicheza mara kwa mara.
MIONGONI mwa mabeki waliopewa nafasi na kocha Manqoba Mngqith na kuitumia vizuri ni beki wa kulia, Ibrahim Kazimoto ambaye alipandishwa timu kubwa kutokea ya vijana ya Yanga U-20.
Kiwango alichokionyesha beki huyo ni kama anatuma ujumbe wa kuamsha ushindani kwenye kikosi cha Yanga ambacho kina mabeki wanne, Kibwana Shomari, Israel Mwenda na Yao Attohoula ambaye amekuwa akicheza mara kwa mara.
Kazimoto ameanza kujitengenezea nafasi hiyo kupitia michezo miwili ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CFFA FC ya Madagascar, ambapo Yanga ilishinda jumla ya mabao 8-1, ikianza na ushindi wa 4-0 ugenini kabla ya kuibuka na ushindi mwingine wa 4-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa Azam Complex, Chamazi, Dar.
Katika michezo hiyo, Kazimoto hakuishia kutimiza majukumu yake ya ulinzi pekee, bali pia alionyesha ubora wa kusaidia mashambulizi, akifunga bao katika mchezo wa marudiano. Bao hilo lilikuja baada ya kusoma vizuri mpira uliopigwa na Mudathir Yahya, kisha kupanda ndani ya eneo la hatari na kuunganisha krosi hiyo kwa kichwa na kuipa Yanga bao la kwanza.
Bao hilo ni ishara ya namna Kazimoto uwezo wake wa kuongeza nguvu katika mashambulizi ya timu, hasa katika soka la kisasa ambalo linahitaji mabeki wa pembeni kupanda na kujenga mashambulizi na kutengeneza nafasi za kufunga, badala ya kubaki nyuma kusubiri kuzuia mawinga.
KIBWANA, ISRAEL KAZI IPO
Yao tayari ameonyesha muendelezo wa kiwango tangu mwishoni mwa msimu uliopita wakati timu hiyo ikiwa chini ya kocha Pedro Goncalves.
Na msimu huu aliendeleza kiwango bora kwenye mechi saba za mwanzo lakini Kibwana na Mwenda bado hawajapata nafasi ya kucheza.
Kwa Kibwana ambaye pia amekuwa akipambana kuwania nafasi ya beki wa kulia, kiwango kinachoonyeshwa na Kazimoto kinaongeza ushindani katika eneo hilo.
Ubora wake unaweza kuwa silaha muhimu, lakini sasa atalazimika kuonyesha kile ana cho we za kuo nge za katika timu, ikiwamo namna ya kusaidia mashambulizi bila kuathiri majukumu ya ulinzi.
Hali hiyo inamfanya Kibwana kuhitaji kutumia kila nafasi atakayopewa na benchi la ufundi kuonyesha ubora wake, hasa katika mchezo wa sasa unaohitaji mabeki wa pembeni kuwa na uwezo wa kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja.
Kwa Mwenda, changamoto ni kuhakikisha anarejea kwenye ushindani wa kupata nafasi ya kucheza. Kadro Kazimoto anavyoendelea kupata nafasi na kuitumia vizuri, ndivyo inavyokuwa muhimu kwa Mwenda kuonyesha kiwango kizuri mazoezini na kuwa tayari anapohitajika.
Hata hivyo, michezo miwili ya kimataifa aliyoonyesha Kazimoto bado ni mapema kuaminisha kuwa tayari ana nafasi ya kudumu kikosini atapaswa kuendeleza kiwango chake.
MZIZE, BOXER
Kiwango anacho onyesha beki huyo huenda akapita njia za vijana wengine ambao waliwahi kupandi shwa kutoka timu za vijana hadi kupewa nafasi timu ya wakubwa.
Baadhi ya wachezaji waliowahi kupitia makuzi ya vijana ni Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye alianza kupata umaarufu Yanga 2018, hasa baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba, Oktoba 2018.
Boxer alicheza kwa mara ya kwanza derby hiyo akiwa amepandishwa kutoka kikosi cha pili cha Yanga na kocha Mwinyi Zahera.
Aliziba pengo la beki Juma Abdul aliyekuwa majeruhi na kumdhibiti winga Shiza Kichuya katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 0-0.
Mwingine ni Clement Mzize aliyepandishwa kutoka kikosi cha vijana 2021/22, lakini alianza kuonekana katika mechi za wakubwa msimu uliofuata wa 2022/23 chini ya kocha Nasreddine Nabi. Mechi yake ya kwanza kucheza ilikuwa Septemba 13, 2022, dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Benjamin Mkapa. Aliingia dakika ya 80 akichukua nafasi ya Farid Mussa, Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-0, msimu uliofuata alifunga mabao matano na kutoa asisti moja kwenye Ligi Kuu, akiisaidia Yanga kutwaa ubingwa. Msimu wa 2023/24 alifunga mabao sita na kutoa asisti saba katika Ligi Kuu. Pia aliibuka mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho kwa mabao matano katika mechi sita, ikiwamo hat-trick. Uliofuata chini ya kocha Miguel Gamondi alifunga mabao 14 na asisti sita kwenye Ligi Kuu akiwa mfungaji bora wa Yanga katika mashindano hayo.
MSIKIE MWENYEWE
Kazimoto anasema: “Nimecheza ligi ya U-20 ina utofauti kidogo na huku Ligi Kuu ambako unapaswa kuongeza kujiamini zaidi makocha mara nyingi wamekuwa wakinitengeneza na kuniamini kuwa naweza kufanya kitu kikubwa.
“Pre season (maandalizi ya mwanzo wa msimu) nimefanya pamoja na timu na nimekuwa nikicheza mechi za kirafiki nafikiri hilo limenisaidia sana kuendelea kuaminiwa na kupewa mechi kwenye kikosi cha Yanga ambacho kina wachezaji wenye uzoefu mkubwa sana.”