Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karibu Mgeusa jiandae kwa majaribu TFF

KATIBU Pict

Muktasari:

  • Kabla alikuwepo bwana Oscar Mirambo ambaye alikaimu kwa muda na baada ya Mgeusa kuteuliwa, yeye amerudishwa katika eneo ambalo amekuwa na uzoefu nalo ambalo ni la ufundi.

KIJIWE kilishtuka kidogo baada ya kuona mkeka ule wa TFF ambao ulitupa jina la Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo la soka ambaye ni bwana Evans Mgeusa anayechukua nafasi hiyo kwa kudumu hivi sasa.

Kabla alikuwepo bwana Oscar Mirambo ambaye alikaimu kwa muda na baada ya Mgeusa kuteuliwa, yeye amerudishwa katika eneo ambalo amekuwa na uzoefu nalo ambalo ni la ufundi.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, ndivyo tunavyotaka kwa Oscar Mirambo kwani kwa muda mfupi alioongoza nafasi ya ukatibu mkuu, amefanya kazi nzuri.

Na hapa kijiweni tunaamini Mgeusa ataendeleza yale mazuri ambayo mtangulizi wake kayafanya na yeye atatupa mazuri zaidi katika soka letu kwa vile nafasi yake ndio ya kiutendaji.

Hata hivyo kwa vile ndio anaanza kutumikia nafasi yake hiyo nyeti, mtaani huku kuna ushauri ambao tunapenda kumpa ili aweze kutumikia nafasi yake kwa mafanikio na asikwame siku za usoni.

Ushauri huo ni kumtaka awe mvumilivu, mwenye hekima na mwenye kusimamia kile kilicho sahihi kuendana na majukumu ya nafasi yake lakini kubwa zaidi amuombe sana Mungu.

Nafasi yake ina majaribu mengi sana ambayo akiweza kukabiliana nayo, atafanikiwa ila kinyume chake, anaweza kuja kuiona nafasi hiyo ni chungu.

Kuna majaribu ya zile timu mbili za Kariakoo ambazo zenyewe zinatakaga kujipangia kile ambacho zinaona kinawapa faida pasipo kujali kama kina faida kwa soka au hakina na kama kipo ndani ya kanuni au hakipo.

Majaribu mengine ni ya watendaji mbalimbali ambao wengine wako ndani ya ofisi yake na pia wale wa nje.

Kuna ambao watataka kujiweka karibu naye sio kwa nia njema ya kuendeleza soka bali kutengeneza mazingira ya kuchuma kupitia huo ukaribu wa kimkakati ambao watalazimisha kuuweka na baadaye mambo kumharibikia yeye.

Uzuri ameshakaa kwenye bolu hivyo ana uzoefu mkubwa na sisi tunaojiita watu wa mpira.